Kisukari huathiri figo

Pamoja na madhara mengi yatokanayo na kisukari ,matatizo ya Figo ni moja ya madhara makubwa yatokanayo na kisukari.Figo inamishipa midogomidogo ya damu ambayo inachuja  uchafu kutoka kwenye damu  .Sukari nyingi kwenye damu inaweza kuharibi mishipa iyo ,kadri muda unavyopita  itapelekea figo kushindwa kufanya kazi yake vizuri na baadae kupelekea Figo kushindwa kufanya kazi kabisa.

Vitu hatarishi vinavyomfanya mtu mwenye kisukari apate matatizo ya figo:

 • Kuwa na shinikizo la damu
 • mafuta mengi kwenye damu
 • Uvutaji Wa sigara na unywaji Wa pombe.

Dalili:

 • Dalili za ugonjwa Wa Figo zinaanza kuoneka miaka 5-10 baada ya tatizo kuanza .dalili izo ni pamoja na
 • Kukojoa Mara kwa Mara wakati Wa usiku  na baadae mchana,kuchoka ,maumivu ya kichwa ,kichefuchefu na kutapika ,ngozi kuwasha  na mwili kujaa maji (miguu , uso na tumbo ).

Kugundua:

Tatizo ili la Figo  linangundulika kwa  kuona protein ya albumin kwenye mkojo ,kwa hiyo mtu mwenye tatizo LA kisukari ni vizuri kufanya uchunguzi Wa mkojo mara kwa mara ili kungundua tatizo ili  mapema maana ugunduzi watatizo mapema unasaidia kuokoa Figo isiharibike zaidi

Namna ya kuepukana na tatizo hili:

 • Njia rahisi ya kujikinga na tatizo ili ni kuhakikisha kiwango cha sukari kwenye damu kipo kiwango sitahiki cha sukari kwenye damu .
 • Kupata mlo kamili.
 • Kufanya mazoezi mara kwa mara .
 • Kunywa maji kwa wingi .
 • Kupunguza kiwango cha  chumvi. anachokula.
 • Kutumia dawa za kisukari ipasavyo .

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show