Kisukari na Uume Kutosimama

Inakadiriwa kwamba asilimia 35-75 ya wanaume wenye kisukari watapata tatizo la kutosimamisha uume kwa kiasi fulani katika maisha yao. Tatizo hilo huwapata miaka 10 hadi 15 mapema zaidi ya wale wasio na kisukari.

  • Tatizo linaweza kuwa kushindwa kabisa kusimamisha uume au uume kushindwa kuendelea kusimama wakati wa kufanya mapenzi
  • Kusimamisha uume inahitaji mishipa ya damu na ya fahamu yenye afya, homoni za kiume na hisia za mapenzi.
  • Sababu za uume kutosimama huchangiwa na kuharibiwa kwa mishipa ya damu, mishipa ya fahamu na misuli ya uume kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu.
  • Ukipata tatizo hili muone daktari maana yeye ndiye atakayejua tiba sahihi kulingana na afya yako na uwezo wako wa kuhimili tiba.
  • Kula vizuri, kuacha matumizi ya pombe na sigara, kufanya mazoezi, kupata usingizi wa kutosha na kupunguza msongo wa mawazo husaidia kuzuia tatizo hilo.

Privacy Preference Center