Kujiandaa na safari ukiwa mgonjwa wa kisukari

Ni muhimu sana kwa mgonjwa wa kisukari kujiandaa kwa ajili ya safari yoyote ambayo anatarajia kwenda.  Kabla ya safari inashauriwa kupata barua kutoka kwa kituo cha afya inayoonyesha kuwa msafiri anaugonjwa wa kisukari, dawa anazotumia pamoja na vifaa kama sindano na mashine za kupimia sukari. Iwapo safari ni ya ndege mgonjwa anapaswa kuwajulisha wahusika wa usalama kuhusu ugonjwa wake na haja ya kubeba dawa hizo na vifaa husika. Inashauriwa kubeba walau mara mbili ya kiasi cha dawa ambacho mgonjwa angetumia ndani ya mda huwo wa safari. Tahadhari hii ni muhimu kwani kuna uwezekano wa kuvunjika kwa dawa kama insulin, kucheleweshwa kwa usafiri au dharura yoyote nyingine ambayo inaweza kupelekea matumizi makubwa zaidi ya dawa. Vile vile kubeba betri za ziada kwa ajili ya mashine ya kupimia sukari kwenye damu ni jambo la muhimu. Inashauriwa mgonjwa aendelee na mpango wa chakula kadri ya maelekezo ya daktari. Na pia abebe vyakula vidogo katika mzigo wake wa mkononi  kama tahadhari pale ambapo akipata dalili za upungufu wa sukari mwilini.  Mgonjwa wa kisukari anashauriwa kusafiri na mtu anaefahamu juu ya ugonjwa wake. Iwapo anasafiri mwenyew inashauriwa atembee na kitu ambacho kinaweza kuonyesha kuwa yeye ni mgonjwa wa kisukari pale inapotokea dharura kama vile kadi ya hospitali.  Kwa watumiaji wa insulin, insulin ambayo mgonjwa amebeba inapaswa kuwekwa mbali na joto wakati wote pamoja na kutumia paketi za barafu ilikuhifadhi ubora wa dawa. Inashauriwa mgonjwa abebe insulin katika mzigo wake wa mkononi ilikuweza kuhakikisha uhifadhi wake ni sahihi. Insulin haipaswi kugandishwa. Katika safari mgonjwa anapaswa kwenda kwenye kituo cha afya akiwa na barua yake pale tu anapopata dalili za kuzidiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center