Homa kwa watoto

Homa ni dalili yenye kutambulika kama joto la mwili kupanda juu ya nyuzi 38Β°C , au kwa kawaida hujulikana kama mwili kuchemka.

Homa ni dalili na sio ugonjwa, hivyo basi inaweza kusababishwa na magonjwa tofauti na hali tofauti katika mwili wa mtoto.

Mtoto anapo pata homa ni ishara kwamba mwili wake unajaribu kupigana na ugonjwa katika mwili inaweza kuwa (maambukizi, vidonda, saratani na mengineyo)

Homa mara nyingi huambatana na dalili nyinginezo zikiwemo;

 • Mtoto kushindwa kunyonya
 • Kupungua hamu ya kula
 • Degedege
 • Kulia sana kwa watoto wachanga
 • Manjano
 • Mwili kukakamaa
 • Kuharisha
 • Kutapika
 • Kikohozi
 • Koo kuwasha
 • Uvimbe sehemu tofauti

Dalili hizi hutokana na dalili husika za ugonjwa uliopelekea mtoto kupata homa.

Homa kwa mda mrefu ina madhara kwenye mwili wa mtoto na huweza pelekea mtoto kupata degedege.

Hivyo basi, mtoto anapokua na homa, ni muhimu kuonana na daktari kwa ajili ya uchunguzi na vipimo zaidi ili kupata matibabu husika ya ugonjwa sababishi.

Katika mazingira ya nyumbani, ni muhimu pia kujaribu kushusha joto la mwili la mtoto kama msaada wa kwanza kusubiri au kuelekea hospiali kwa njia zifuatazo;

 1. Punguza nguo alizo vaa au zilizo mfunika mtoto. Abaki na nguo nyepesi
 2. Unaweza mkanda kwa kitamba cha maji baridi au vuguvugu
 3. Unaweza mpa mtoto paracetamol kulingana na maelekezo ya mfamasia utakapo nunua dawa. Dozi hutofautina na umri wa mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center