Jinsi ya kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na shinikizo la damu

 

Kwa sababu magonjwa ya moyo huanza taratibu na kukaa muda mrefu bila kuonyesha dalili, hivyo ni vema tukachukua hatua mapema ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Vifuatavyo ni vitu vya muhimu kuvifanya ili kujikinga nayo;
1.Jenga tabia ya kufanya mazoezi kwa utaratibu maalum. Inashauriwa mtu kufanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku au kufanya kazi ambazo zitaushughulisha mwili ili kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
2. Kula mlo sahihi. Ulaji wa vyakula vyenye kiwango kidogo cha mafuta kama nafaka zisizokobolewa, matunda na mboga za majani zimeonyesha kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Pia kupunguza matumizi ya chumvi yaliyokithiri hasa ikiwa mbichi.
3. Punguza unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara. Unywaji wa pombe usiofuata taratibu za kiafya na uvutaji wa sigara uliokithiri umeonesha kuwa ni chanzo cha kuibua magonjwa ya moyo.
4. Kupunguza uzito kwa walio wanene (obese). Utafiti unaonesha kupunguza uzito kwa mazoezi au kurekebisha ulaji kwa wale wanene kunapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa kiasi kidogo.
5.Kujiepusha na msongo wa mawazo(depression) na wasiwasi unaozidi kiasi (anxiety). Utafiti unaonesha msongo wa mawazo na wasiwasi uliozidi inachangia kwa kiasi fulani mtu kupata magonjwa ya moyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center