Sababu zinazoweza kusababisha magonjwa mbalimbali ya moyo

Magonjwa ya moyo yako katika makundi mbali mbali yakiwemo yafuatazo: Mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio stahiki, Kufeli kwa moyo, Moyo kutokupata damu ya kutosha, Magonjwa ya valvu za moyo, Maambukizi katika moyo, Hitilafu za moyo za kuzaliwa nazo na mengineyo mengi.

Zifuatazo ni sababu zinazoweza pelekea kupata au kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

-Umri mkubwa; Umri kadri unavyokuwa mkubwa ndivyo mishipa ya damu inavyozidi kuharibika na kuwa dhaifu na misuli ya moyo pia hutanuka.
-Jinsia; Wanaume wana hatari ya kupata matatizo ya moyo zaidi kuliko wanawake, lakini kwa upande wa wanawake hatari huongezeka baada ya kuacha kupata siku zao.
-Historia ya magonjwa ya moyo katika familia pia humfanya mtu kuwa katika hatari ya kupata matatizo ya moyo, kwa mfano shinikizo la damu na moyo kutanuka.
-uvutaji sigara; uvutaji sigara husababisha kuharibika kwa kuta za mishipa ya damu na kuongeza uwezekano wa mafuta kujishikiza kwenye kuta zake na kuzuia damu kupita vizuri matokeo yake shinikizo la damu linaweza kutokea na pia shtuko la moyo.
-Vyakula; Vyakula vya mafuta,chumvi nyingi hasahasa chumvi mbichi hupelekea matatizo ya moyo, kwa mfano kukosekana kwa oksijeni kwenye moyo na shinikizo la damu.
-Kisukari; Kisukari pia kisipotibiwa vyema kinapelekea matatizo ya moyo.
-Uzito uliozidi pia unaongeza hatari ya matatizo ya moyo.
-Ukosefu wa mazezi; Hupelekea mafuta mengi kubakia kwenye mwili hivyo kama matokeo matatizo ya moyo hutokea.
-Ukosefu wa usafi wa kutosha; Hii inaweza pelekea ya vimelea mbalimbali vinavyoathiri moyo kama vile bakteria na virusi.
-Maambukizi kwa mama mjamzito; Maambukizi ya virusi kama vile “Rubella” husababisha kuzaliwa kwa watoto wenye tundu katika moyo.

Zipo sababu nyingine pia zinazosababisha magonjwa ya moyo kama vile kubadilika kwa vina saba,ulevi kwa kinamama wajawazito(Inaathiri mtoto ambaye hajazaliwa),madawa mbali mbali,magonjwa ya mfumo wa hewa na mengineyo mengi.

Kuwa pamoja nasi katika ukurasa wetu kwa Elimu zaidi na tutakujuza mengi zaidi, tunahimiza pia kuuliza maswali pale ambapo panahitaji ufafanuzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show