Zifahamu sababu za jino kung’olewa

Kung’oa jino ni aina moja matibabu ya matatizo ya meno lakini hii inashauriwa iwe suluhisho la mwisho kabisa baada ya matibabu mengine ya meno kushindikana.Hii ni kwasababu meno yana umuhimu sana katika kazi za kila siku za kinywa pamoja na kuchangia katika munekano mzuri wa mtu.

Zifuatazo ni sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea jino kung’olewa:

 • Jino kutoboka sana kiasi kwamba linasababisha maumivu makali yasiyoweza kutibika kwa kujaza jino.
 • Matatizo ya fizi yanayosababisha kulika kwa mfupa unaoshikilia meno na kufanya meno kulegea na kupelekea kung,olewa
 • Kwa ajili ya matibabu ya kupanga meno vizuri ambapo kuna baadhi ya meno yanabidi yatolewe ili mengine yasogee na kukaa vizuri mdomoni.
 • Meno kuvunjika na kubaki vipisi vidogo au mizizi tu
 • Maandalizi ya kutengeneza meno bandia ambapo baadhi ya meno ambayo hayatatumika au yamelegea yatatolewa
 • Meno yaliyozidi ndani ya kinywa,yaani kua na meno zaidi ya 32
 • Meno yanapofika muda wa kutoka na bado hayapo kinywani na yamekaa vibaya ndani ya mfupa ni ya kung’olewa pia
 • Meno yaliyopo kwenye mstari amabapo taya limevunjika
 • Kutoa meno ya utotoni mda wake unapofika ili kuruhusu meno ya ukubwani kuota
 • Uvimbe  au kansa ya taya inayosababisha baadhi ya meno kulegea na hivyo kutolewa
 • Meno yaliyopo kwenye eneo ambalo litatibiwa kwa mionzi.

Hivyo basi unashauriwa usingoje hadi pale jino litakapofika wakati ambapo matibabu ya kung’oa ndo suluhisho pekee bali ujitahidi kutunza meno yako maana yana umuhimu sana.Muone daktari wa meno mapema kuepuka kua kibogoyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center