Msaada wa haraka kwa aliyemwagiwa chemikali machoni

Aina hatarishi za kemikali kwenye macho zimegawanyika katika makundi makuu mawili, nazo ni; alkali mf. Baking powder, sabuni za kuogea na kusafisha masinki, n.k kundi la pili ni tindikali(acid) mf. Vinegar

MUATHIRIKA AFANYE YAFUATAYO;
1. Safisha macho kwa maji mengi ya kutiririka kwa muda usiopungua dakika 30. Mf, kimbilia bafuni na ufungulie bomba kwenye macho huku ukiinua ngozi ya kope ili maji yaingie ndani.
2. Safisha mikono kwa kutumia maji na sabuni ili kuhakikisha kemikali hazibaki mkononi.
3. Kama muathirika ni mvaaji wa lensi ya macho(contact lens) azitoe kama hazikutoka baada ya kuosha kwa maji.
TAHADHARI.
-Asipikiche macho
-Usiweke kitu chochote machoni zaidi ya maji. Mf dawa za macho, nk
-Mkimbize mgonjwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center