Huduma ya kwanza kwa mtu anayepatwa na degedege

Degedege ni hali ya ghafla ya kutingishika kwa mwili mzima au miguu na mikono pia huambatana na kukaama kwa misuli ya mwili. Hali hii uhusishwa na magonjwa ya ubongo kama kifafa, majeraha katika kichwa, vichocheo vya kwenye damu kama upungufu wa sukari, upungufu ya oksijeni, kushuka kwa shinikizo la damu na homa ya degedege.

huduma ya kwanza kwa mtu anayepatwa na degedege ni kuhakikisha mazingira salama hadi pale anapotulia, iwapo utashuhudia mtu ana patwa na degedege fanya yafuatayo:

  • Kuwa mtulivu na hakikisha wale wote waliowazunguka wanakuwa watulivu.
  • Usijaribu kumzuia mgonjwa kwa kumkandamiza au kuishika mikono na miguu.
  • Ondoa vitu vyote vyenye ncha kali au vigumu vinavyoweza kumdhuru mgonjwa.
  • Mfungue nguo au kitu chochote kilicho kwenye shingo ambacho kinaweza kuathiri upumuaji.
  • Msaidie mgonjwa alale upande na uweka kitu laini mfano nguo iliyokunjwa chini ya kichwa cha mgonjwa
  • Baki na mgonjwa hadi degedege litakapokoma lenyewe na usimpulizie hewa mdomoni. Fanya hivyo iwapo hataweza kupumua baada ya degedege kukoma.
  • Onesha upendo wakati mgonjwa anaporudiwa na fahamu na iwapo ataonekana kuzidiwa, omba msaada na mwahishe mgonjwa katika kituo cha afya kilicho karibu.

1 thought on “Huduma ya kwanza kwa mtu anayepatwa na degedege

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center