Uhusiano wa mazoezi na matumizi ya dawa muhimu

Dawa hutumika kwa minajili ya kuimarisha afya ya mtu kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya ambayo mtu anaweza kuwa anakabiliana nayo katika mzunguko wa maisha ya kila siku, Mfano kutuliza maumivu ya kichwa, tumbo, mgongo, kifua nk.

Mazoezi ya viungo vya mwili yanaweza kutazamwa kwa namna moja au nyingine kama moja ya dawa zenye uwezo wa kuimalisha Afya ya mtu, hii ndio sababu watu hushauriwa kufanya mazoezi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Kama kawaida kila dawa huwa na matokeo fulani katika mwili(side effets), matokeo haya huweza kuwa matokeo chanya au hasi kulingana na aina ya dawa, hali ya afya ya mtumiaji na maelekezo ya matumizi ya dawa husika ingawa lengo kubwa la kutumia dawa ni kupata matokeo chanya(yaani kuimarisha afya).

Dawa tunazotumia(Kumeza, kunywa au kuchoma) huwa na matokeo mbalimbali kama; Kupotea kwa hamu ya kula, Kizunguzungu, kuishiwa nguvu za mwili, Kuongezeka kwa mapigo ya moyo na mzungo wa damu, kuongezeka kwa joto la mwili na pengine kupungua ufanisi wa utendaji kazi katika mfumo wa fahamu(hii hupelekea wengine kupoteza fahamu). Mazoezi nayo huwa na matokeo yake kama kuongeza joto la mwili, kuongeza kiwango cha kutoa taka mwili(hususa kwa njia ya jasho), kuongeza matumizi ya nguvu mwilni na kuongeza mahitaji ya gesi ya oksijeni katika mwili.

Kwa kuwa dawa za kawaida zina matokeo yake na mazoezi pia yanamatokeo yake, hivyo mtu anayefanya mazoezi ili hali anatumia dawa fulani anaweza kupata madhara mbalimbali kiafya endapo hapatakuwa na uwiano maalumu kati ya mazoezi anayofanya pamoja na dawa anazotumia.

Kuongezeka kwa matatizo ya moyo, kuharibika figo, kupoteza fahamu, kuishiwa nguvu na pengine kupoteza maisha ni miongoni mwa madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtu anayefanya mazoezi huku anatumia dawa mbalimbali.

Kuna baadhi ya dawa zinahitaji maji mengi mwilini, zinahitaji mtu awe amekula chakula vizuri na pia apate muda wa kutosha kupumzika, hivyo unapokuwa unatumia dawa hizi huku unafanya mazoezi ambayo yanapelekea kupoteza maji mwilini, kuongeza matumizi ya chakula kwa ajili ya kuzalisha nguvu mwilini na pia kuuchosha mwili unakua unaingilia utendeji wa dawa hizi ndani ya mwili.

Mazoezi ni njia ya muhimu na salama katika harakati za kuimarisha afya ya mtu, lakini endapo mtu anatumia dawa mbalimbali basi hana budi kufanya mazoezi chini ya usimamizi maalumu wa mtaalamu wa Afya hususa mtaalamu wa mazoezi ya viungo(Physiotherapist), hii itasaidia kupunguza/kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na muingiliano wa matokeo ya mazoezi na dawa kwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show