Kuziba na kubadilisha mwonekano wa meno

 

Ifahamu vizuri huduma ya kuziba na kubadilisha muonekano wa  meno,huduma hii inapatikana katika kliniki zote za meno,hivo unapomtembelea daktari wa meno wapaswa kutambua aina  za matibabu unayoweza kupata na kuchagua aina ya matibabu kwa kushauriana na daktari.

Huduma hii inatolewa kama:

 • Jino limetoboka,huleta karaha kwa mabaki ya chakula kukwama na wakati mwingine husababisha maumivu
 • Jino limekatika au kuvunjika,mfano kung’ata mfupa na kuvunja jino,au kuanguka na kuvunja meno.
 • Meno yana rangi isiyompendeza mwenye nayo,mfano baadhi ya watu kutoka mikoa ya arusha,shinyanga na Kilimanjaro huwa wana rangi Fulani kwenye
 • Kuboresha mwonekano wa meno yako mfano,kuweka metali za rangi kama dhahabu na fedha au kufanya meno yako yawe meupe zaidi na kuziba mwaya.

Faida za huduma hizi

 • Kurudisha mwonekano mzuri wa jino hasa meno ya mbele na kumpendezesha mtu
 • Kumaliza kabisa maumivu katika jino husika kama lilishaanza kuuma
 • Kusaidia jino kuweza kuendelea kutafuna vzuri
 • Kuepusha kung’oa meno na kuzuia mtu kuwa kibogoyo hapo baadaye
 • Kusaidia sehemu ya jino iliyotoboka kurejea kwa kiasi Fulani

 

Matokeo hasi ya huduma hizi

 • Sehemu ya jino kuondolewa ili kuweza kuweka dawa/risasi zinazotumika kuziba hivo jino linapungua uimara kwa kiasi Fulani
 • Gharama kubwa ambazo baadhi ya watu hawawezi kumudu
 • Matibabu haya huchukua muda kidogo hivo unaweza kupangiwa tarehe ya kurudi na inashauriwa umalizie matibabu
 • Risasi inaweza kuondoka baada ya muda Fulani hivo utahitaji kufanyiwa huduma hii tena.

Inashauriwa unapohisi kuwa jino lako limetoboka ni vyema kuliziba hata  kabla halijaanza kuuma,lakini ni vigumu kujua kama jino limetoboka kama hujafanyiwa uchunguzi na wataalamu,jenga tabia ya kuchunguzwa meno yako.

LINDA TABASAMU LAKO.

1 thought on “Kuziba na kubadilisha mwonekano wa meno

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show