Mzunguko wa hedhi,jua kuhusu siku salama na siku hatarishi.

Mzunguko wa hedhi ni nini?

Ni idadi ya siku unazochukua kwanzia siku ya kwanza unapopata hedhi hadi siku ya kwanza ya mzunguko unaofuatia.

 Siku za hatari ni nini?

Siku za hatari ni siku ambazo unaweza kupata mimba ukifanya tendo la ndoa kwa yule asiyetaka kupata mimba.Kama wewe unatafuta mimba huwezi kuita siku za hatari au danger days, kwa kuwa wewe huna hatari yeyote ya kutaka mimba.Maneno haya hutumika na wale tu wasiotaka kupata mimba, kwa hiyo wanakwepa kabisa wasipate mimba. Hivyo huziita siku za danger au za hatari.

JINSI YA KUTAMBUA SIKU ZA HATARI ZINGATIA HAYA.

  1. Mbegu ya kiume huishi kwa zaidi ya masaa 72 yani siku 3+
  2. Yai la mwanamke (ova) huishi kwa masaa 24
  3. Tambua mzunguko wako ni wa siku ngapi,kwa kawaida ni 21-35.
  4. Tambua jinsi ya kuhesabu siku ambayo yai linatoka kwenye ovaries (ovulation).Hii ni Rahisi unachukua siku za mzunguko wako unatoa 14.

Ili ukwepe kabisa kabisa usipate mimba basi chukua mzunguko wako tafuta siku ya Kutolewa yai (ovulation) halafu ongeza siku 4 mbele na kutoa siku 4 nyuma ya mzunguko. Yaani kama

una mzunguko wa siku 30 unafanya hivi 30-14 = unapata 16 halafu unatoa na 4 unapata 12 alafu 16 unaongeza na 4 unapata 20.Kwa hiyo siku ya kwanza ya hatari kwako ni siku ya 12 ya mzunguko wako wa hedhi na siku ya mwisho ya hatari yako ya kupata mimba ni siku ya 20. Unaweza jiuliza kwa nini uwe na wasiwasi na siku 4 baada ya yai kutoka? Kumbuka hizi ni hesabu tu,kiukweli mwili wako unaweza badilika saa yeyote na wiki yeyote na kujikuta siku zako za uzazi zinabadilika, na kama ulikuwa hutaki kupata mimba ukajishtukia unapata.

Kwa hiyo kwa mzunguko wa siku 30 uliokamilika.

  1.  siku ya kutungwa mimba ni siku ya 16(fertilization)
  2. siku za uzazi ni siku ya 12,13,14,15,16 na 17
  3.  siku za hatari ni kuanzia siku ya 12hadi ya 20
  4. Siku zote zilizobakia ni siku salama yaani siku ya 1 hadi ya 11, siku ya 21hadi ya 30.

 

4 thoughts on “Mzunguko wa hedhi,jua kuhusu siku salama na siku hatarishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show