Kisukari na Tatizo la Fangasi

Fangasi huweza kumuathiri mtu yeyote na mara nyingi husababishwa na fangasi aitwaye “Candida albicans”. Hupenda kushambulia zaidi sehemu za mwili zenye mikunjo, hali ya joto na unyevunyevu kama vile uke na chini ya maziwa kwa wanawake, kuzunguka kucha, katikati ya vidole vya mikono na miguu, kwapani, katikati ya mapaja, kona za mdomo na chini ya govi(foreskin) kwa wanaume wasiotahiriwa.

Watu wenye kisukari hasa wale wasio na udhibiti mzuri wa sukari mwilini wana hatari kubwa ya kupata mambukizi ya fangasi kwa kiwango kikubwa na mara kwa mara ukilinganisha na wale wasio na kisukari.

Hali hii husababishwa na kwamba;

  1. Kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu husababisha kutolewa kwa sukari iliyozidi kupitia jasho, mkojo na ute. Fangasi hupenda sukari na hivo kuongezeka kwa ukuaji wao maeneo yenye maji maji hayo.
  2. Sukari nyingi kwenye damu pia huzuia kinga ya mwili kufanya kazi kwa ufasaha na ndiyo maana watu wenye kisukari hushindwa kupigana na maambukizi ya fangasi.

Fangasi zishambuliapo mwili husababishwa muwasho na ngozi kuwa nyekundu ;wakati mwingine huambatana na vijipu vidogo vidogo au magamba na maumivu.

Ikiwa kwenye uke dalili huwa ni muwasho, maumivu kama ya kuungua na moto, kutokwa uchafu unaofanana na jibini(cheese) au harufu mbaya.

Uonapo dalili hizo unashauriwa kumuona Daktari ili aweze kuhakikisha kwamba tatizo hilo ni fangasi au maambukizi mengine na atakupa tiba sahihi kulingana na tatizo lako.

2 thoughts on “Kisukari na Tatizo la Fangasi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center