Nilikatwa mguu kwa sababu ya kisukari

Calvin aliketi akiwa amevaa vazi la hospitali na mguu wake ukiegeshwa kwenye kitanda cha hospitali. Yeye alifunga safari kutoka nyumbani kwake nakuenda mara moja kwenye Hospitali ya karibu baada ya kuona mguu wake umevimba.

Calvin Alikuwa akisafisha vidonda vidogo kwenye mguu wake kwa wiki sasa, kutumia spirit, kutumia mafuta na hata bandage. Alidhani alikua anapata nafuu.

Lakini jopo la madaktari ambao waliingia ndani na kutoka katika chumba hiki cha uchunguzi, kuangalia na kutathmini, waliona hali yake haikuendelea vizuri. “Labda wangeweza tu kukata vidole vichache”, alidhani hivo Calvin. Lakini uchuunguzi haukuonesha hivyo. Mguu ulianza kuoza.

“Kusema ukweli, Calvin, hakuna kingine tunaweza kukusaidia,” Calvin alikumbuka daktari akisema. “Ni ama kuutoa mguu wako, au utafariki.”

Calvin alishangaa. Alikuwa na ufahamu juu ya kisukari na alijua matatizo yanaweza kutokea kutokana na ugonjwa huo. Lakini vitu vilienda ghafla na hapakuwa na wakati wa kusubiri.

“Basi wakati gani tunaaenda?” Calvin aliuliza.

“Sasa,” alisema daktari.

Daktari alipoondoka chumbani kwa Calvin mwenye umri wa miaka 49, Calvin alilia na kumpigia mama yake simu.

“Maisha yangu hayatakua sawa tena,” alisema kwa sauti ya majonzi.

“Lakini angalau nipo hai.”

Calvin ni kati ya mamilioni ambao wamegunduliwa na ugonjwa wa kisukari na ambao wamekuwa na adhari za kisukari kama hizi za kuoza kwa mguu.

Ni vizuri kwa wagonjwa wenye kisukari kupima sukari yetu kwenye damu mara kwa mara na kumeza dawa kama ilivyoelekezwa na daktari. Na kwa wasioumwa ni vizuri kuzingatia dalili za kisukari ili kuepuka na matatizo kama haya.

1 thought on “Nilikatwa mguu kwa sababu ya kisukari

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center