Uhusiano kati ya kuota meno na kuharisha kwa mtoto

Hatua ya kuota meno kwa mtoto wakati mwingine huwa ngumu sana kwa mtoto mwenyewe na mzazi pia. Meno ya kwanza huanza kutokea kuanzia miezi mitano hadi miaka miwili japo kuna wanaowahi na kuchelewa zaidi ya hapo.

Dalili za mtoto kuota meno ni kama mtoto kuanza kung’ata fizi ,kupenda kuweka vitu mdomoni,kukosa usingizi,kukosa hamu ya kula, kulia sana na mate kujaa mdomoni.Kumekuwa na imani potofu kuwa meno ya mtoto yanapoota husababisha kuharisha kwa mtoto au joto la mwili kupanda lakini mpaka sasa hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha vitu hivi viwili.

Sasa kwanini wazazi wanaamini kuna uhusiano kati ya hivi vitu????

  • Mtoto anapoanza kuota meno huwa na tabia ya kuokota vitu ovyo na kuweka mdomoni ili kupunguza ile hali ya fizi kuwasha na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kula vijidudu vinavyosababisha kuharisha.
  • Pia ni katika umri huu ambapo mtoto huanza kula vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama na hivyo kama chakula hakijaandaliwa katika mazingira ya usafi kinaweza kusababisha maambukizi ya vijidudu hivi vya kuharisha
  • Imani hii potofu imefanya magonjwa mengi ya mfumo wa chakula kupuuziwa na kushindwa kutibiwa kwasababu wazazi wengi wanaamini kwamba kuota kwa meno ndo kunasababisha kuhara kwa mtoto.
  • Hivyo basi unapoona mtoto wako anaharisha mara kwa mara wakati meno yanaota hakikisha kuwa anatafuna vitu visafi,anywe maji mengi na apewe vyakula vitakavyopunguza hali hii. Hali hii ikiendelea mpeleke mtoto kwenye kituo cha afya haraka kupatiwa matibabu,meno hayasabishi mtoto kuharisha,wajulishe na wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center