Fizi zangu zinatoa damu nifanyaje?..

Je, fizi zako zinatoa damu?..

Tatizo la fizi kutoa damu

 Baadhi ya watu wamekuwa wakitokwa na damu kwenye fizi  hasa wanapopiga mswaki  au kung’ata vitu kama matunda au hata kutafuna nyama.Watu wengi hasa kwa nchi kama Tanzania hawana tabia ya kuchunguza mate wanayotema hasa wakiwa wanapiga mswaki,hii husababisha watu wengi kutokugundua tatizo hili mapema, unashauriwa kuwa na tabia ya kuchunguza mate yako hasa unapopiga mswaki hii itakusaidia kugundua tatizo mapema.

download (1)

Sababu ni nini?..

 • Hatua za mwanzo za magonjwa ya fizi:Pale bakteria waliopo mdomoni wanaposhambulia mabaki ya chakula na kusababisha maambukizi kwenye fizi,fizi zinavimba na kutoa damu.
 • Upungufu wa vitamin C na baadhi ya madini chumvi mwilini.
 • Tabia ya kusaga meno kwa nguvu hasa wakati wa usiku(bruxism).
 • Matumizi ya tumbaku(kutafuna au kuvuta sigara).
 • Msongo wa mawazo.
 • Mpangilio mbovu wa meno.
 • Kuwa na ugaga kwenye meno.
 • Kuchangia mswaki na mtu mwenye magonjwa ya fizi.

Ufanye nini kutatua tatizo..

 • Safisha meno yako kwa umakini hakikisha unaondoa uchafu wote kila siku.
 • Sukutua kwa maji ya uvuguvugu yenye chumvi kidogo kwa sekunde kadhaa mpaka dakika moja angalau mara mbili kwa siku baada ya kupiga mswaki,tatizo likiendelea moune daktari.
 • Kula matunda na mbogamboga kwa wingi.
 • Epuka kuchangia mswaki na mtu hata mtu wako wa karibu.
 • Punguza msongo wa mawazo.
 • Acha kuvuta sigara au kutafuna tumbaku.
 • Usilazimishe vijiti vya kusafishia meno kuingia katikati ya meno.
 • Jitahidi kuacha kutafuna meno na kuyasagasaga hasa unapokuwa na hasira au wakati wa kulala,msaada wa kitaalamu wa kudhibiti tatizo hili unapatikana kwa daktari wa meno.
 • Ukiona una uchafu wa rangi ya maziwa,njano,nyeusi au kijani kwenye meno pata msaada kutoka kwa daktari wa meno,upatiwe huduma ya kusafisha kitaalamu maana uchafu huu huwa hautoki kwa mswaki.
 • Pata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya ya kinywa chako.
 • Waweza kutumia dawa zinazorejesha vitamin mwilini(multivitamins) kama umeshauriwa na daktari.

USHAURI...

Tatizo hili huwa ni hatua za mwanzo za magonjwa ya fizi,kama halitatibiwa linaweza kusababisha magonjwa sugu ya fizi ambayo husababisha kupata majipu kwenye fizi,fizi kulika na meno kuonekana marefu zaidi,kupata mwaya ambao haukuwepo zamani,meno kutikisika na kuanguka yenyewe na hata kula mfupa wa taya na kulifanya taya kukosa uimara wake,ni vizuri kutibiwa mapema kuepuka matatizo haya.
flaviana nyatU
Upcoming dentist..

kwa ushauri kuhusu afya ya kinywa na meno,wasiliana nasi 0688-636-717

2 thoughts on “Fizi zangu zinatoa damu nifanyaje?..

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center