Fahamu kuhusu Iskemia sugu katika miguu

Nini maana ya iskemia?

-Iskemia hutokea endapo damu inayofika katika sehemu ya mwili ni kidogo(au kutokufika) na kusababisha seli kuathirika kwa kukosa oksijeni hivyo kupelekea kufa kabisa kama hali ikikaa muda mrefu. Hali hii hutokea katika sehemu mbalimbali za mwili kama vile mikono,miguu,moyo n.k

-Iskemia ya miguu hutokea kama damu isiyo ya kutosha inapofika katika mguu au damu isipofika kabisa.

-Zifuatazo ni sababu zinazoweza kusababisha iskemia sugu katika miguu

  • Uvutaji sigara
  • Kisukari
  • Shinikizo la damu
  • Mafuta mengi mwilini

-Dalili za Iskemia ni kama zifuatazo

  • Misuli ya kigimbi(utasi) kukaza wakati wa kutembea
  • Maumivu wakati ya miguu wakati wa kutembea na maumivu huisha pale anapoacha kutembea, pia huongezeka anapotembea kwenye sehemu iliyoinuka na haitokei akiwa amekaa(intermittent claudication). Maumivu haya hutokea kwenye kigimbi,paja na hata matako.
  • Kadri muda unavyozidi kwenda vidonda(ulcerations) vinaweza kutokea au mguu kubadilika rangi na kuwa mweusi(gangrene).

-Hivyo basi kwa watu wenye tatizo la kisukari na shinikizo la damu wanahitaji uangalizi makini na uzingatiaji wa matibabu ili kuepusha tatizo hili. Inashauriwa kiafya pia kwa wavuta sigara kuacha na wenye mafuta mengi mwilini kupunguza kwa njia mbalimbali kama mazoezi.

-Uonapo dalili za iskemia ya miguu tembelea kituo cha afya ili uweze kuchunguzwa zaidi na kupata matibabu maana kuna matatizo mengine yanayofanana na iskemia.

2 thoughts on “Fahamu kuhusu Iskemia sugu katika miguu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center