Jinsi ya kujua kama una tatizo la shinikizo la damu( Hypertension) na viashiria vyake.

Tunaweza sema mtu ana tatizo la shinikizo la damu pale ambapo msukumo wa damu ( blood pressure)  huwa juu kwa muda mrefu, juu ya 140/90mmHg au chini ya hapo pale endapo mtu atakua anatumia dawa kwa ajili ya shinikizo la damu.

Shinikizo la damu hupitia hatua mbali mbali za awali kabla ya kuja kugundulika na tatizo hilo. Hatua zinaweza kuwa kama ifuatavyo:

Presha ya kawaida huwa chini ya 120/80mmHg.

Kidokezo cha presha kuanza kupanda (120-139)/(80-89)mmHg

Hatua ya kwanza ya shinikizo la damu (140-159)/(90-99)mmHg

Hatua ya pili ya shinikizo la damu 160/100mmHg au Zaidi

Mara nyingi dalili za shinikizo la damu huanza kujitokeza pale ambapo presha ya mwili ipo hatua ya kwanza juu ya 140/90mmHg, ndipo mtu huanza kujisikia uchovu usio na sababu ya msingi, kichwa kuuma, kifua kuuma, kupumua kwa shida,kukohoa, kizunguzungu, na dalili nyinginezo zinzoambatana na magonjwa ya moyo.

Shinikizo la damu ni moja kati ya magonjwa yasiyoambukizwa, ila kwa takwimu za shirika la afya la dunia ( WHO) linaonesha takribani watu zaidi ya bilioni moja duniani kote wanakabiliwa na tatizo hilo.

Hivyo, inashauriwa kuwa na mazoea ya kupima presha mara kwa mara ili kujua mapema endapo kutakua na viashiria vya shinikizo la damu na kuchukua hatua stahiki.


Joseph Mwalongo MD5

Saving patients life is my pleasure

All author posts

Privacy Preference Center