Mazoezi ya Viungo Katika Kuimarisha Afya

Vituo vya mazoezi ya viungo vimekuwa vikiongezeka sana katika maeneo mengi ya miji kwa ajili ya kutoa huduma hizi kwa watu katika kujiweka imara na kujenga ukakamavu wa mwili. Vituo hivi vinavyojulikana kama Gym Centers, vimekuwa pia hata katika sehemu za mitaa ambapo watu wamekuwa wakienda na kujiimarisha katika kuwa na uimara wa mwili. Vituo hivi vimekuwa na mchango mkubwa sana si katika kuwa sehemu za kuingizia watu vipato. Ila faida kubwa ni kuwa kama vituo vya kujiimarisha kwa mwili wenye nguvu na kuufanya kuwe na utimamu wa mwili.

Kuna faida nyingi sana za kiafya Katika nidhamu ya kila siku ya watu wanaoenda kufanya mazoezi haya mbali na kuonekana kuwa na mjengo mzuri wa vifua na misuli. Kiafya zifuatazo ni sababu muhimu kwanini Mazoezi haya yana umuhimu mkubwa kwa mhusika;

1. Ni njia ya Kuondosha Hofu na Msongo wa Mawazo.

Katika kufanya mazoezi kunasaidia sana utokaji wa kemikali ya dopamine inayosaidia sana Katika kuweka mwili katika ya utulivu na kupelekea kumjengea mtu kuwa na ujasiri Katika utendaji kazi wa kila siku katika kufanya maamuzi. Kwa kuwa pia kunakuwa na utulivu mkubwa hivyo kunakuwa na mazingira epushi na msongo wa mawazo.

2. Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Moyo

Ni dhahiri mazoezi haya yanasaidia sana kuchoma mafuta ambayo huwa ni mazingira hatarishi ya Magonjwa wa moyo kutokea. Hivyo Katika muda wa ufanyaji Mazoezi haya mafuta mwilini hupungua kwa njia ya oksijeni ambapo huepusha viashiria chochezi vya Magonjwa ya moyo. Na si pekee moyo pia kufanya mazoezi haya ya viungo ni kupunguza kitambi kama kero ya watu wengi ila pia dalili mbaya kiafya.

3. Huimarisha Usingizi Mzuri

Mazoezi huufanya mwili utulie katika mifumo mbalimbali Katika mwili, na hivyo pia husaidia upataji mzuri wa usingizi na kwa njia ya upataji mzuri wa usingizi kunaepusha hali ya mfadhahiko na kupoteza ufanisi katika kazi.

4. Hukuza Afya ya Akili

Kwa kuwa kipindi cha Kufanya mazoezi kinaambatana na mifumo ya upumuaji na mzunguko wa damu kuwa vizuri na oksijeni kufika vizuri katika mfumo wa Fahamu. Kwa njia hii husaidia Maendeleo mazuri ya ubongo na kumpa mtu Nafasi kubwa ya kuimarika katika afya ya akili.

5. Huimarisha Misuli na Kufanya Mwonekano unaovutia

Hili nalo huvuta watu wengi sana katika kuwa katika vituo hivi vya Mazoezi kuimarisha misuli na kutengeneza maumbo ya kuvutia kimwonekano. Na neno six packs hutafutwa sana na watu wengi katika vituo hivi. Mwonekano mzuri wa mwili kutokana na mazoezi haya unampa mtu ujasiri na hivyo kusaidia ufanisi katika utendaji wa kazi mbalimbali.

Wakati huu ni muhimu sana ukatenga muda wako katika kufanya mazoezi ya viungo, hata kama si katika vituo husika unaweza jitengenezea eneo dogo kisha ukajenga nidhamu ya kujiimarisha kimazoezi kila siku. Afya ni utajiri, na mazoezi ya viungo ni kwa afya yako.

© Raymond Nusura Mgeni 2018, Md 5
+255 676 559 211

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show