Mazoezi yapi hayaruhusiwi au sio salama kwa mama mjamzito wakati wote wa kipindi cha ujauzito wake?

Mazoezi kila siku ni bora kwa ajili ya afya yetu na ni moja ya ushauri tunaopatiwa na wataalamu wa afya. Mama mjamzito pia anapaswa kufanya mazoezi ili kujikinga na baadhi ya magonjwa kama presha ya kupanda, kisukari, kifafa cha mimba, kupata tatizo wakati wa kujifungua, ila kuna baadhi ya mazoezi yakifanywa na mama mjamzito yanaweza kuhatarisha afya yake na ya mtoto kwa ujumla na mazoezj yenyewe ni yafuatayo:

1. Mazoezi yanayohusisha kuanguka mara kwa mara.

2. Mazoezi yanayohusisha kuligonga tumbo la mama mjamzito pamoja na mazoezi yanayohusisha kushikana, kusukumana.

3. Mazoezi yanayohusika kuruka au kupita juu ya vizuizi.

4. Mazoezi yanayohusisha kuruka viunzi huku unajivuta sehem za juu ya mwili.

5. Mazoezi yanayohusisha Kuzungusha kiuno ukiwa umesimama.

6. Kufanya mazoezi kwa wakati mrefu ghafla na kukaa kipindi kirefu bila ya kufanya mazoezi.

7. Kufanya mazoezi eneo lenye joto kali/ jua pia na eneo lenye hali ya unyevu nyevu.

8. Usishikilie pumzi ndani wakati wa mazoezi.

9. Usifanye mazoezi mpaka utakapofikia hali ya kuchoka kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center