UNAJUA KAMA MAZOEZI NI TIBA?!

Wengi wetu tumekua tukifanya mazoezi kama mazoea au utamaduni ila kutokana na tafiti nyingi za kitaalam zimeweka wazi kua mazoezi yanaweza kua tiba sahihi kwa baadhi ya magonjwa bila kutumia dawa. Baadhi ya magonjwa hayo ni haya yafuatayo

1. KISUKARI: Kama ijulikanavyo ungonjwa wa kisukari ni moja kati ya magonjwa hatarishi na yanayoongoza kwa vifo hasa kwa watu walioenda umri, lakini imeelezwa kua kufanya mazoezi mara kwa mara hukuza misuli na kuzuia sukari kuhifadhiwa kama mafuta ambayo ndiyo yanayoleta shida kwnye ugonjwa wa “kisukari”, pia mazoezi hayo husaidia kuongeza usikivu wa seli mwili zetu juu ya kichocheo Kitolewacho na kongosho kiitwacho insulini kinachoweka sukari katika kiasi sahihi mwilini.

2. PUMU: Pumu ni moja ya magonjwa yanayojulikana na kusababisha vifo kutokana na mwili kukosa hewa oksijen ya kutosha, mazoezi ya mara kwa mara yanayohusisha utumiaji wa mapafu na moyo kwa wingi yanasaidia kuyaimarisha mapafu na kuzuia kupata ugonjwa wa pumu bila kusahau mazoezi haya yasifanyike sehemu za baridi wala kwenye maeneo yenye vumbi, moshi au vichochezi vyovyote vya ugonjwa huu.

3. MAUMIVU YA UNGIO ZA MIFUPA(JOINT): Huu ugonjwa unawapata watu wa umri ulioeenda na kupeleka kukunja au kunyoosha mguu kuwa vigumu na kuambatana na maumivu, hivyo kufanya mazoezi yanayohusisha kukimbia au kunyoosha viungo hasa vya hizo maungio inapunguza tatizo hili

3. TATIZO LA MOYO: Mazoezi yanayohusisha moyo kufanya kazi zaidi yanasaidia kuuimarisha na kutumia hewa oksijeni ya kutosha hivyo moyo huwa imara na kuweza kufanya kazi yake ipasavyo na kutuepusha na tatizo hili mara kwa mara

KUMBUKA-Mazoezi haya yanaendana sambamba na aina ya mlo unaotumia epuka vyakula hatarishi kwa ugonjwa na usiache kutumia dawa kwa uangalizi wa daktari

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show