Tatizo la ugaga kwenye meno(dental calculus)

Ugaga kwenye meno ni uchafu sugu ambao una mkusanyiko wa mamilioni ya bacteria ambao hushambulia mabaki ya chakula na uchafu uliopo kwenye meno na kutoa kemikali ambazo huungana na madini mbalimbali yaliyoko kwenye mate naย  kutengeneza uchafu mgumu kama sumenti kwenye meno.

Ugaga huu pia unaweza kutokea kwenye vishikizi ย vya meno bandia,unaweza kuwepo juu tu ya fizi yaani sehemu inayoonekana kirahisi au ukawepo ndani chini ya fizi ambako haunekani mpaka matumizi ya vifaa maalumu kama periodontal probes, kifaa hiki huingizwa kwa umakini na daktari ndani kidogo ya fizi na yeye huweza kutambua kama kuna uchafu uo,zipo njia nyingine ambazo zinaweza kutumiwa na daktari kugundua uwepo wa ugaga.

Yafuatayo ni madhara ya kuwa na ugaga(dental calculus) kwenye meno.

 • Kutokwa damu kwenye fizi wakatiย wa kupiga mswaki au kungโ€™ata vitu kama matunda.
 • Husababisha harufu mbaya mdomoni
 • Kusababisha kutoboka kwa meno kwani ugaga huficha uchafu na bacteria
 • Kuwa na visehemu wazi kati ya jino na fizi
 • Husababisha kulika kwa fizi na kufanya meno kuonekana marefu kuliko kawaida
 • kusababisha mwanya ambao haukuwepo zamani
husababisha kutokea mwanya ambao haukuwepo zamani na fizi kulika hivo meno huonekana marefu kuliko kawaida.
 • Hupelekea magonjwa sugu ya fizi ambayo yasipotibiwa mapema husababisha mfupa wa taya kulika na kusababisha meno kulegea na kuanza kuanguka yenyewe.
 • Kutunga usaha kwenye fizi(kutengeneza vijipu)ย ambavo huleta maumivu na wakati mwingine homa.

ufanye nini endapo tayari una tatizo hili?

 • Endeleza juhudi zako za kusafisha kinywa vizuri angalau mara mbili wa siku,usisahau kusafisha ulimi wako mara zote.
 • Wasiliana na daktari wa meno mpange ratiba ya kwenda kusafisha meno kwani ugaga hauwezi kutoka kwa njia ya mswaki ni lazima kusafisha meno hospitalini.
 • Fuata maelekezo utakayopewa na daktari kabla na baada ya kusafisha meno.

Usikubali kuendelea kutembea na ugaga kwenye meno yako tafuta huduma kwenye kliniki ya meno iliyo karibu na wewe,jali afya ya kinywa chako tunza tabasamu lako.

meno na fizi zenye afya…

Flaviana Nyatu DDS 5 ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

A happy and passionate dental surgeon.

All author posts

Privacy Preference Center