Vitamini A na ujauzito

Kipindi cha ujauzito wanawake hujitahidi kula kwa wingi vyakula vyenye virutubisho kama madini na vitamini sana. Hii ni muhimu kwa ajili ya afya zao na utengenezwaji mzuri wa viumbe walivyobeba. Pamoja na faida hizo kuna baadhi ya virutubisho vikizidi sana huleta madhara., mfano vitamini A.

Vitamini A ni virutubisho vinavyoongeza kinga ya mwili, husaidia macho kuona vizuri. Ni muhimu katika uzazi na utengenezwaji wa viungo kama moyo, mapafu na figo.

Kuna aina mbili za vitamini A.
1. Vitamini A iliyokwisha tengenezwa ( preformed)
Hii hupatikana kwenye vyakula vitokanavyo na wanyama kama vile maini, nyama, mayai na bidhaa za maziwa. Aina hii ya vitamini A ikizidi kwa mama mjamzito husababisha matatizo katika maumbile ya mtoto ,hata kupelekea upofu na matatizo ya maumbile. Hivyo ni muhimu kuhakikisha mama mjamzito hali sana maini , akila ale kidogo tu. Pia vidonge vya vitamin A kwa mama mjamzito vitumike kwa uangalizi mkubwa kuepuka madhara haya.
2. Vitamin A ambayo haijatengenezwa ( provitamin) . Hii hutokana na vyakula kama mboga za majani, karoti , viazi vitamu n.k Hii ni salama ukilinganisha na aina ya kwanza. Hivyo mama mjamzito anaweza jipatia vitamini A kutoka kwa vyakula kama karoti, brokoli , viazi vitamu na mboga za majani.

1 thought on “Vitamini A na ujauzito

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center