Fahamu sababu hatarishi za saratani ya tezi dume

Saratani ya tezi dume ni aina ya saratani inayotokea katika tezi dume.Tezi dume hupatikana kwa mwanaume tuu.Tezi dume hukaa sehemu ya chini baada ya kibofu cha mkojo.Tezi dume hufanya kazi ya kuzalisha majimaji laini(seminal fluid) ambayo hutumika katika kusafilisha mbegu za kiume.

Sababu hatarishi za saratani ya tezi dume

  • Umri mkubwa.Uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume huongezeka umri unapoongezeka,umri wa miaka zaidi ya 50 huongeza zaidi hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
  • Historia katika familia.Kama katika familia baba au kaka ana ugonjwa huu uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume huongezeka mara mbili zaidi.
  • Unene kupindukia.Unene kupindukia huongeza hatari ya kupata saratani ya tezi dume
  • Mazoezi.Ufanyaji mazoezi hupunguza hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
  • Magonjwa ya zinaa.Magonjwa ya zinaa kama kisonono huongeza hatari ya kupata saratani ya tezi dume kuliko mtu ambaye hajawahi kupata magonjwa ya zinaa.
  • Uvutaji wa sigara.Tafiti zinaonyesha uvutaji wa sigara unahusishwa na kupoteza maisha kwa wagonjwa wa saratani ya tezi dume.

Fanya uchunguzi wa awali (PSA TEST)mara kwa mara kuepuka madhara yatokanayo na saratani ya tezi dume

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center