Zijue dalili za mwanzo za kisukari na wakati sahihi wa kumuona daktari kwa ajiri ya vipimo na ushauli

Kisukari ni ugonjwa ambao kuna ongezeko kubwa la sukari aina ya glukozi katika mzungo wa damu na hivyo kupelekea mwili kutofanya kazi sawa na husababisha madhara mbalimbali nje na ndani ya mwili.
Mara upatapo dalili zifuatazo ni muhimu kumuona daktar wako kwa vipimo na ushaur zaidi

β€’ kiu cha mara kwa mara (hii hutokea hata wakati wa usiku mtu anaamka na kunywa amji zaidi ya mara moja kwa usiku mmoja)
β€’ njaa kali hata baada ya kula
β€’ kupata haja ndogo mara kwa mara ( unaweza gundua hii hali kwa kuchunguza umeamka mara ngap usiku kwa ajili ya kupata haja ndogo ukilinganisha na siku za nyuma)
β€’ uchovu wa mwili pasipo kufanya kazi nzito
β€’ kuchelewa kupona kwa vidonda na majeraha madogo ukilinganisha na kawaida
β€’ mate kukauka mdomoni bila sababu
β€’ kupungua uwezo wa kuona (kuona ukungu)
β€’ kupungua uzito
β€’ kizunguzungu
β€’ maambukizi ya magonjwa ya ngozi
β€’ ganzi la miguuni na vinjani mwa mikono
β€’ kupungua nguvu na hamu ya tendo la ndoa hasa kwa wanaume

1 thought on “Zijue dalili za mwanzo za kisukari na wakati sahihi wa kumuona daktari kwa ajiri ya vipimo na ushauli

  1. Bora ungetujuza nini sukari ya kawaida,ipi sukari isiyo ya kawaida,lini kuna hatari, vipi kuepuka kisukari, nini kufanya kisikupate n.k.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center