Je, mgonjwa wa kisukari anaruhusiwa kutumia kilevi?

Mgonjwa wa kisukari anaruhusiwa kunywa kilevi lakini iwe kwa kiasi, yani kinywaji kimoja au viwili kwa wanaume na kinywaji kimoja kwa mwanamke kwa siku. Kinywaji kimoja ni sawa na bia moja au glass ya wine moja au 50mls za pombe kali (kama inavyoonekana kwenye picha chini). Katika mpango wa chakula kinywaji kimoja kinahesabika kuwa na gramu 15 za wanga na hivyo ni muhimu kumjulisha Daktari wako juu ya matumizi yako ya pombe ili aweze kuihesabia katika kalori zako za siku.

Unywaji wa pombe kwa kiasi hichi kwa wagonjwa wa kisukari inapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo ila kuzidisha kiasi hichi humuweka mgonjwa katika hatari ya kupata vipindi vya sukari kushuka au kupanda pamoja na kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na figo. Inashauriwa kunywa kilevi pamoja na chakula ili kuzuia sukari kushuka, hali ambayo huletwa na kilevi.

Unywaji wa kilevi masaa ya usiku haishauri kwani humuweka mgonjwa katika hatari ya kupata kipindi cha sukari kushuka wakati amelala, jambo ambalo ni hatari kwani mgonjwa hayupo katika hali ambayo anaweza kuhisi dalili za hali hiyo.

Matumizi ya vilevi huweza kuingiliana na dawa mbali mbali za kisukari ikiwemo insulin na dawa zingine za kisukari zinazotumika kwa njia ya kinywa. Matumizi ya Chlorpropamide na kilevi inasababisha “Disulfiram like reaction” ambayo inaambatana na kushuka kwa presha, kushindwa kupumua, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na dalili zingine hatarishi. Hivyo ni jambo la muhimu sana kwa mgonjwa wa kisukari kuwa muwazi kuhusu matumizi yake ya kilevi ya awali na baada ya kubainika kuwa anakisukari.

Katika hatua flani za ugonjwa wa kisukari hasa pale ambapo matatizo mbali mbali yanayohusiana na ugonjwa yanapotokea matumizi ya kilevi yanakuwa hayaruhusiwi kabisa kwa mgonjwa. Hivyo inashauriwa kuhudhuria kliniki mara kwa mara ilikuweza kupata ushauri sahihi kwa wakati utakao linda afya ya mgonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center