Kisukari na Mtoto wa Jicho

Mtoto wa jicho ni tatizo ambalo lensi asilia ya jicho inakuwa na ukungu. Lensi hairusu mwanga kupita ipasyavyo na pia mwanga hauakisiwi vizuri kwenye retina. Matokeo yake mtu anaona ukungu, picha ya kitu kuharibiwa na kuona gizagiza.

Mtoto wa jicho anaweza kusababishwa na mabadiliko ya jicho yatokanayo na kubadilika kwa umri (uzee), madawa, upasuaji wa jicho, ajali ya jicho na magonjwa kama kisukari.

Jinsi gani kisukari kinasababisha mtoto wa jicho!?

Lensi inapokea virutubisho kutoka kwenye majimaji yaliyoko sehemu ya mbele ya jicho(aqueous humor). virutubisho hivyo ni Pamoja sukari na kwa mtu ambaye anatatizo la kisukari na hafanyi hatua za kuhakikisha sukari ipo kwenye kiwango cha sukari kwenye damu kinacho sitahiki ,sukari inakuwa nyingi kwenye majimaji hayo na kwenye lensi pia.Kiwango kikubwa cha sukari kwenye lensi kitasababisha lensi kujaa maji(kuvimba).

Kwenye lensi kuna kimengenya kinachobadilisha sukari ya kwenye damu kuwa sorbitol. Sorbitol ikijikusanya kwenye lensi inafanya lensi iwe na ukungu na baadae mtoto wa jicho.

Ufanye nini ili kujilinda na mtoto wa jicho!?

Kwa mtu mwenye kisukari ni lazima ahakikishe ana kiwango sitahiki cha sukari kwenye damu kwa kufanya mazoezi, kutumia dawa ipasavyo ya kisukari na kuwa na mlo kamili .
Kumtembelea daktari wa macho mara kwa mara kwaajili ya uchunguzi wa macho

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center