Nile nini endapo nina Kisukari!? (part 2)

Vyakula vipi vinanifaa!?

Waweza kudhani kwamba kuwa na kisukari maana yake ni kuishi bila vyakula uvipendavyo. Habari njema ni kwamba bado waweza kuendelea kupata vyakula hivyo ila kwa kiwango sahihi. Hakikisha mlo wako unatengenezwa na makundi yote ya vyakula.

Makundi ya vyakula ni yapi!?

  1. ย Mbogamboga; zinaweza kuwa
    I) Zenye wanga mfano viazi, mahindi na njegere.
    II) Zisizo na wanga mfano nyanya, pilipili hoho, pilipili, karoti.
  2. Matunda mfano machungwa, matikiti, matufaha(apples), ndizi, nanasi, zabibu n.k
  3. Nafaka “zisizokobolewa” mfano ngano, mahindi, ulezi, mtama, uwele, mchele. Waweza pia kula tambi au mikate.
  4. Protini mfano minofu ya nyama, nyama ya kuku au bata isiyo na ngozi, mayai, samaki, maharage makavu, karanga n.k
  5. Mafuta salama mfano mafuta ya mimea kama alizeti na mzeituni (olive oil), parachichi, karanga na mbegu.
  6. Bidhaa za maziwa sisizo na mafuta mfano maziwa yenyewe, jibini na mtindi.

Nahitaji kula kiasi gani!?

Njia rahisi ya kupanga mlo wako ni kupitia njia ya sahani (Plate method); hii ni njia nzuri hasa kwa chakula cha mchana na cha usiku.
Tumia sahani yenye upana wa inchi 9; nusu ya sahani weka mbogamboga zisizo na wanga, robo ya sahani weka nyama au protini ya aina yeyote na robo iliyobaki weka nafaka au mbogamboga zenye wanga. Hivi husindikizwa na bakuli au kipande cha tunda na glasi ndogo ya maziwa.

Privacy Preference Center