Pneumonia/nimonia au homa ya mapafu kwa watoto

Nimonia ni ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na vitu vingi na unaweza uka dhuru watu wa umri tofauti ingawa unaonekana Zaidi kwa watoto kulinganisha na watu wazima. visababshi vya nimonia kwa mara nyingi hutofautiana kutegemea na umri wa mtoto kwanzia anapo zaliwa.

visababishi vya nimonia vinaweza kugawanywa katika makundi mawili makubwa; maambukizi ya vidudu na visababishi visivyo tokana na maambukizi.

visababishi vitokanavyo na maambukizi ni kama virusi, bacteria, fungi ambavo hufikia mapafu kutokana na kuvuta hewa chafu yenye vidudu hivi au kupitia maambukizi katika damu

visababishi visivyotokana na maambukizi ni kama chakula kuingia katika mfumo wa hewa na vinginevyo

kwa kawaida ili mtoto apate nimonia, inabidi hawa wadudu waweze kuizidi nguvu kinga ya mwili ya mtoto; kinga hutokana na antibodies kutoka kwa mama au chanjo, na uwezo wa kusafisha njia ya hewa.

dalili za nimonia

 1. kuhema haraka (huhesabiwa katika kumchunguza mtoto na mtumishi wa afya)
 2. sehemu ya chini ya kifua kuingia ndani anapo hema
 3. kukohoa
 4. homa
 5. kushindwa kunyonya au kula

Inashauriwa uonavyo dalili yoyote hapo juu kumfikisha mtoto hospitali kwa ajili ya uchunguzi Zaidi. mtoto anaweza hitaji X-RAY ya kifua, vipimo vya damu ingawa mara nyingi dalili hutosha kusema mtoto ana nimonia

nimonia huwa katika makundi kuu matatu kulingana na ukali

 1. nimonia ya chini
 2. nimonia ya wastani
 3. nimonia kali

nimonia ya chini mtoto anaweza akatibiwa na dawa za kunywa nyumbani kama hatakua na maradhi mengine. nimonia ya wastani na kali zina hitaji uangalizi Zaidi na dawa za kuchoma katika mishipa (sindano) na pia anaweza akahitaji kuwekewa oxigeni.

nimonia ya chini huchukua matiabu ya kati ya siku 3 hadi 5 za dawa. nimonia za wastani na kali huhitaji pia siku 5 hadi 7 za dawa na matibabu mengineyo.

NAMNA YA KUZUIA NIMONIA

 1. Hakikisha mtoto wako amepata chanjo zake zote
 2. nguo za baridi
 3. kuepuka sehemu zenye msongamano
 4. nyonyesha kwa usahihi
 5. uchunguzi wa mara kwa mara kliniki au hospitali

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center