Fahamu juu ya kifaa pandikizwa cha kusikia (cochlear implant)

Kwa mara ya pili madaktari nchini Tanzania wamefanikiwa kupandikiza kifaa cha kusaidia kusikia.
Wanufaika wa huduma hii ni watoto wadogo haswa wasioweza kusikia kwa kiwango kikubwa au kutosikia kabisa.
Kifaa hiki husisimua moja kwa moja mishipa inayohusika na kusikia .
Mtoto mwenye kuwekewa kifaa hiki,ataweza kutambua sauti tofauti tofauti katika mazingira hivyo kumsaidia kusikia kadiri anavyokuwa.
Takwimu zinaonyesha kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 5 wanazaliwa na tatizo la kutosikia.
Hivyo tunapaswa kupeleka watoto hospitalini ili kubaini tatizo mapema.

Privacy Preference Center