Huduma ya kwanza kwa aliyezama majini

Katika huduma ya kwanza, Kuzama ni pale ambapo mtu anashindwa kupumua kwasababu kinywa na mdomo vimezama ndani ya maji au kimiminika kingine. Mtu anayezama majini anaweza asiwe na fuko na kutapatapa kama inavyoonekanaga katika filamu.

A. Ita msaada. Kama kuna mtu karibu aje kukusaidia, au tuma mtu akaite msaada ili unapohitajika uwepo.

B. Msaidie muathirika kutoka kwenye. Isipokuwa kama ni mtoto aliyezama au wewe ni mtaalamu wa kuokoa watu majini (lifeguard), haushauriwi kuelekea katika kina kirefu cha maji kwaajili ya kumuokoa mtu huyu. Kwani mtu anapozama majini huwa na nguvu sana kiasi cha kuweza kukujeruhi na kukuzamisha nawe pia. Cha kufanya; chukua kamba ndefu au fimbo na umrushie ili aishike, na kisha umvute kutoka kina kirefu na kumweka nchi kavu. Unaweza kufungia kitu mwishoni mwa kamba ili muathirika aweza kuikamata kamba vizuri.

C. Huduma ya kwanza.

Baada ya kumtoa muathirika majini unaweza kufanya yafuatayo.

  1. Kama hajapoteza fahamu na anakohoa, mhamasishe akohoe ili kusaidia kutoa maji kwenye njia ya hewa na mapafu.
  2. kama amepoteza fahamu au hajiwezi. Chunguza kama anaweza kupumua kama ifuatavyo; weka sikio lako mdomoni kwake na usikie kama hewa unatoka, pia tazama kama kifua kinapanda na kushuka. Pia tazama kama ana majeraha yoyote dhahiri.
  3. Kama anapumua mlaze kwa ubavu kama ilivyoonyeshwa katika picha hapa chini, huku ukihakikisha kwamba mdomo wake unabaki wazi ili kuruhusu maji yatoke.

    Namna ya kumuweka mtu aliyezama majini kuruhusu maji yatoke kinywani
  4. Kama hawezi kupumua, mlaze chali na ‘ikiwezekana’ mpe pumzi za mdomo kwa mdomo (mouth to mouth breathing) kwa kubana pua yake na kumpulizia kwa nguvu(kama ni mtu mzima) au taratibu kwa mtoto. Mpe pumzi hizi mara nne kisha tazama tena kama anapumua.
  5. Waweza kurudia hatua ya 3 na 4 hadi muathirika atakapoweza kupumua au msaada zaidi utakapopatikana.
  6. Ni muhimu sana kumpeleka muathirika hospitali hata kama akipata nafuu, kwaajili ya matibabu zaidi maana anaweza kupata athari za muda mrefu kama pneumonia, matatizo ya moyo, na pia anaweza kuwa amepata majeraha yasiyoonekana kirahisi.

Muhimu: Kuna haja ya msingi sana ya muokoaji kujikinga na magonjwa mengine ambukizi kama VVU (HIV), virusi ya Homa ya manjano (hepatitis B virus) na mengineyo hasa wakati wa kumpa mgonjwa pumzi. Hivyo usimpe pumzi mtu usiyemfahamu au kujua afya yake bila kutumia vifaa maalumu vya kujikinga.

 

2 thoughts on “Huduma ya kwanza kwa aliyezama majini

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show