Maelekezo, nguzo muhimu ya matumizi sahihi ya dawa.

Tabia ya kutozingatia vitu vya msingi inazidi kushika kasi miongoni mwa watu walio wengi, sio tu katika maswala ya Kisiasa na Elimu bali hata katika maswala ya msingi yahusuyo Afya. Mitazamo duni ya kimaisha inafanya wengi kuyachukulia mambo ya msingi kiuwepesi na matokeo yake wengi huishia kulia na kulaumu.

Katika uwanja wa Afya, tabia ya matumizi ya dawa za muhimu bila kufata maelekezo inazidi kushamili licha ya msisitizo uliopo juu ya matumizi sahihi ya dawa. Maelekezo yamekua yakitolewa na wahudumu wa Afya sambamba na zoezi na ugawaji dawa, maelekezo kama โ€œtumia dawa mara tatu kwa siku kwa muda wa siku saba, tumia maji mengi unywapo dawa, kula vizuri kabla ya kunywa dawa na usiingie kulala mara baada tu ya kunywa dawaโ€ hutolewa yakiwa na maana kubwa sana na kila mtu anapaswa kuzingatia ili kuboresha Afya, lakini walio wengine hawayazingatii.

Miongoni mwa maelekezo yasiyozingatiwa ni lile la kumaliza dozi, tabia ya kutokumaliza dozi huchochewa na sababu mbalimbali kama; mtu kujisikia vizuri(kujiskia kama amepona), uchungu wa dawa(dawa nyingi huwa na radha chungu), dozi kuwa ya muda mrefu sana au pengine kuhitajika kutumia kiwango kikubwa cha dawa kila mara anapotumia dawa. Unakuta muda wa dozi pengine ni siku kumi na nne, lakini kutokana na moja ya sababu tajwa hapo juu mtu anatumia dawa kwa siku tano au saba kulingana na anvyojisikia, tabia hii ni hatari kwa afya na ina madhara mbalimbali.

Miongoni mwa madhara haya ni;

1.Kutokupona kwa ugonjwa(hii inatokana na uwezekano wa kuwepo kwa masalia ya vijidudu vya magonjwa mwilini) na kufanya ugonjwa kushika mwilini(Chronic disease).

2.Kukua na kusambaa kwa tatizo la usugu wa madawa dhidi ya vimelea vya magonjwa, kutokana na dawa kutokuwepo kwa kiwango cha kutosha kumaliza vijidudu vyote( hii ni matokeo ya mfumo wa viumbe kujibadili, kujishikiza na kuzoea mazingira- ( mutation).

Madhara haya yanamatokeo hasi katika Afya ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima kwa ujumla hususa ni pale vijidudu sugu vya dawa vitakapoambukizwa kwa mtu mwingine, mwisho wa siku jamii nzima itakua na tatizo hili. Ni vyema jamii ikajifunza matumizi sahihi ya dawa kwa kuzingatia maelekezo ili kuweza kutunza Afya ya jamii nzima.

Privacy Preference Center