Maumivu ya kifua yaitwayo Angina pectoris

Angina pectoris ni maumivu makali upande wa kushoto wa kifua ambayo hupanda mpaka shingoni, shavuni, mkono wa kishoti hata mpaka mgongoni. Huu sio ugonjwa bali ni dalili ya magonjwa ya mishipa ya moyo.

Mara nyingi maumivu haya huwapata wazee kuanzia miaka 50 na kuendelea wanaosumbuliwa na mafuta kwenye mishipa ya moyo

Angina imegawanyika katika aina kuu tatu
1. Inayotokea mtu akifanya kazi ngumu au akitembea zaidi ya mita 100
2. Maumivu yatokeayo wakati wa kutembea chini ya mita 100 au kufanya kazi kidogo tu au kuoanda ngazi ghorofani
3. Maumivu yatokeayo wakati mtu amekaa na kupumzika tuu.
Maumivu yote haya yanatokana na moyo kuongezeka kazi lakini damu yenye oksijeni haitoshi kwasababu ya mafuta yaliyoganda ndani ya mishipa ya damu

Nini cha kufanya mtu akipatwa na haya maumivu
– Acha shughuli zote na upumzike
– Kama uko ndani, fungua madirisha ya nyumba ili upate hewa ya kutosha
– Siku zote tembea na vidonge vya nitroglycerin kwaajili ya kuondoa maumivu
– Jaribu kuacha tabia hatarishivkama kunywa pombe kali, kuvuta sigara, kutembea kwa kasi, kula vyakula vya mafuta,chumvi au wanga kwa sana
– Epuka hali ya baridi kali au joto kwa sana

2 thoughts on “Maumivu ya kifua yaitwayo Angina pectoris

 1. Funzo zuri, japo ni maswali mawili…

  1. Umesema maumivu haya hutokea upande wa kushoto wa kifua… Je ina maana hayatokei kabisa upande wa kulia au katikati wa kifua?
  2. Je kwa mtu anayepata maumivu upande mwingine wa kifua ambao sio wa kushoto kuna jina lake au ni maumivu tu ya kawaida?

  1. 1. Maumivu yanatokea zaidi upande wa kushoto kwa sababu mishipa ya fahamu ya moyo imesambaa sana upande huo Lakini maumivu haya yanaweza kutokea upande wowote wa kifua, mgongoni na shingoni upande wa kushoto, Lakini inategemea na mishipa ipi ya damu artery imekosa oksijeni kwa muda mrefu hii husababisha ukali wa maumivu kutofautiana.

   2. Sio maumivu yote ya kifua ni ishara ya ugonjwa wa moyo. Unapaswa kuzungumza na daktari wako pale unapopata maumivu ya kifua hasa ya muda mrefu. Lakini aina ya maumivu unayopata inaweza kusaidia sababu ya maumivu hayo. Hivo ni vzuri kumwelezea daktari ni aina gani ya maumivu unayapata labda yanachoma,ya kupwita au kama kuungua,Kwa kawaida maumivu makali na ya kuchoma yanaweza kuhusisha mshipa mkubwa wa damu yaani aorta . Maumivu yanayohusiana na kupumua ndani na nje au kuhofia na kupiga chafya (pleurisy) yanaweza kuhusishwa na magonjwa ya mapafu. Sababu nyingine pia ni pamoja na kucheua kemikali kutoka tumboni ambayo husababishwa na mmeng’enyo mbovu wa chakula au hali wa uoga uliopitiliza.. lakini maumivu yato ya kifua yanahitaji uchunguzi wa kitaalamu ili kujua tatizo ni nini hasa.
   Ishi bila maumivu,kuwa na furaha

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show