Ujue uhusiano mkubwa uliopo kati ya shinikizo la damu (hypertension) na matatizo la figo

Kwa kawaida figo na moyo ni viungo ambavyo vinauhusiano mkubwa sana katika ufanyaji kazi wake na endapo kimoja wapo kikiwa kimepata hitilafu huathiri ufanyaji kazi wa mwenzake.

Presha ya mwili ya iliyo juu (high blood pressure) isipodhibitiwa kwa muda mrefu huathiri figo kwa kiasi kikubwa, hivyo kupelekea kushindwa kufanya kazi yake ya kusafisha taka ndani ya mwili.

Endapo presha haitadhibitiwa kwa muda mrefu mtu anaweza pata dalili za figo kushindwa kufanya kazi ambazo ni pamoja na kubadilika kwa kiasi kikubwa cha mkojo anaoupata kwa siku,mwili kuvimba hasa miguu na magoti.
Pia mtu anaweza kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu, kutapika,kichwa kuuma, kuhisi kuchanganyikiwa, kukosa usingizi, mwili kuwasha na maumivu ya kifua na wakati mwingine kupumua kwa shida. Ikumbukwe hizi dalili huambatana na presha ya mwili kuwa juu.

Hivyo inashauriwa kwa wagonjwa wa shinikizo la damu (hypertension) kutumia dawa na kuzingatia masharti kama alivyoelekezwa na daktari ili kupunguza hatari ya kupata shida ya figo.

Endapo mtu atapata dalili zozote kati ya hizo hapo juu ni vema akafika katika kituo cha afya au hospitali kwa vipimo na matibabu zaidi.

2 thoughts on “Ujue uhusiano mkubwa uliopo kati ya shinikizo la damu (hypertension) na matatizo la figo

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show