Uliza Swali Unalopenda tukuelimishe

Je unaswali ungependa kutuuliza kuhusu mada yoyte ya afya? Leo siku ya Jumanne tunawapa fursa ya kuuliza maswali. Ingia katika comment na uulize swali lako leo. Tutatoa majibu ya maswali. Karibuni sana. 😊

16 thoughts on “Uliza Swali Unalopenda tukuelimishe

  1. Saratani ya Ini si ugonjwa wa kuambukiza. Ni ugonjwa utokanayo na visababishi vingi baadhi vyake vikiwa ni maambukizi ya virusi vya homa ya ini (hepatitis). Sababu nyingine ni kunywa pombe nyingi kwa mda mrefu, kuvuta sigara. Virusi vya homa ya ini ndio njia kubwa ya maambukizi ipelekayo kupata saratani ya ini ikiwa haijatibika. Virusi hivi huambukizwa kupitia ngono isio salama, uchangiaji damu na majimaji mengine ya mwili kutoka kwa mtu alie na maambukizi.
   Namna ya kujikinga na Saratani ya ini
   1. Usinywe pombe
   2. Usivute sigara
   3. Ngono salama
   4. Kupunguza uzito wa mwili
   5. Kupima mara kwa mara afya yako

 1. je matumizi ya dawa za maumivu za diclofenac kwa muda wa miez 6 mfululizo kwa mgonjwa aliyevunjika mguu( femur fracture) yana madhara yoyote?

  1. Matibabu ya mtu alivunjika mfupa katika mwili huwa kwa kawaida hayahisihi dawa zs maumivu kwa mda mrefu angalao siku 3 hadi saba. Maumivu hupungua kabisa yenyewe kama mgonjwa amepata tiba sahihi kutoka hospitali.
   Diclofenac ya mda mrefu inaweza pelekea maudhi mengine kama
   1. Vidonda vya tumbo
   2. Shida katika figo.
   Vi vizuri huyu mgonjwa akarudi hospitali kwa ajili ya kuangaliwa zaidi kama bado anapata maumivu na nini ndo sababu husika. Ili kupata tiba sahihi
   Karibu

 2. Naumwa misuli ya mikono na niguu,napia navimba joint za vdole vya mikono navimba magoti na navimba jointi za miguu kila sehem inayovimba inakua namaumivu makal saaana kias kwamba uwa nashindwa hata kutembea wala kufanya kaz yoyote nina mwaka sasa niko kwenye shidaa hii,tatizo uwa linadum ata miez 3 kisha linapotea,nimeangaika saana hosptali mbalimbali nimepima xley na vpimo vya dam pia nimepimwa sono wajaona tatizo je ninini hki naomben ushaui napata shida hasa wakat wa barid ndo ugonjwa huzid

  1. Pole Bahati, kwa bahati mbaya sijajua una umri gani.
   ila maumivu ulivyo yaelezea yanaonekana kuwa maumivu yatokanayo na ugonjwa mwingine.
   baadhi ya magonjwa au maradhi yanayoweza kusababisha maumivu kama yako yaweza kuwa
   1. sickle cell (siko seli)
   2. rheumatoid arthritis (ugonjwa unao husisha viungo katika mwili)
   3. gout
   kutegemea na umri wako, bado Bahati utahitaji kuonana na daktari kuweza kupata historia ndefu ya ugonjwa wako, na kufanya baadhi ya vipimo vya damu kubainisha ni shida gani ulionayo.
   kwa sasa ni muhimu kuweza kupata ushauri mapema na dawa za maumivu, epuka baridi kwa kuvaa nguo za joto kipindi cha baridi, punguza nyama nyekundu (nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo) na punguza mazoezi mpaka utakapo pata ushauri zaidi ktuokana na vipimo na pia jitahidi kunywa maji mengi zaidi.
   Asante

  1. Kuna aina tofauti za discharge zinazo weza kupatikana katika uke, kwa kawaida discharge katika uke inatakiwa kuwa ya wastani, isokua na harufu, na inakua clear.
   Discharge zisizo kua za kawaida huwa zinakua na rangi tofauti mfano, nyeupe, njano, kijani au mchanganyiko na damu. Pia zinakua na harufu mbaya, na zinatoka kwa wingi mkubwa.
   Discharge hizi zinaweza kutokana na aina tofauti za magonjwa katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Mfano
   1. Maambuki ya magonywa ya zinaa
   2. Saratani ya shingo ya kizazi
   Hivyo basi ni muhimu uonapo discharge inayo ambatana na dalili hapo juu ukaonana na daktari kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi.
   Karibu

 3. I was recently diagnosed with an autoimmune condition, lupus. Tangu kupata taarifa hiyo nimegundua kwamba watu wengi hawajui lupus ni nini and that has made this experience very isolating and no one understands. Why is it like that? And what can we do to increase awareness? Also, lupus kwa kiswahili ni nini? Thanks.

  1. Lupus or systemic lupus erythromatosis kwa kiswahili hufahamika kama ugonjwa wa mfumo wa kinga ya mwili.
   Ni ugonjwa unaotokea baada ya mfumo wa kinga ya mwili kuanza kushambulia baadhi ya viungo mwilini kama figo na vingine.
   Haufahamiki sana kwani ni mara chache kugundulika kutokana na kuwa na dalili ambazo zinafanana na magonjwa mengine.
   Ugonjwa huu hutokeaa hasa kwa watu wazima hasa wanawake. Hutokea mara nyingi kwa waafrika japo madhara yake sio makubwa kama ikitokea kwa jamii ya wazungu.
   Katika kuongeza ufahamu tunaweza tumia siku ya lupus duniani ambayo huazimishwa kila tarehe 10 ya mwezi wa tano kila mwaka katika kutoa elimu na kuchangia kuongeza ufahamu.
   Shukrani.

 4. Habari.
  Kuna rafiki yangu anasumbuliwa n kidole gumba cha mguuni. Kimevimba sana adi kinazidi size ya vidole vingine. Halii hii imempata kwa miaka miwili sasa na kinaenda kikiongezeka. Anpata maumivu pia kwenye hicho kidole.
  Amejaribu kwenda hosiptali mbali mbali lakini wansema hawaoni tarizo.
  Naomba msaada hapo

  1. maumivu katika kidole gumba yanaweza sababishwa na vitu tofauti mfano:
   1. ajali iliohusisha kidole husika
   2. kucha kukua kwenda chini hivyo kukandamiza nyama za kidole
   3. maambukizi ya wadudu kama fungus, na bacteria
   kwa shida iliokaa kwa mda mrefu inawezekana ikawa ni shida ya kucha kukua kwenda ndani katika pembezoni mwa kidole.
   asikate tamaa kwenda hospitali kwani bado anahitaji kuchunguza kwa kina katika kidole husika kupata chanzo cha maumivu yake. ni vyema akaweza kupata ushauri tofauti moja kwa moja kutoka kwa daktari atakae muona

 5. Habari, napenda kuuliza nini chanzo kinachopelekea mtu kuweza kuwa ana sinzia kwa muda mrefu na njia zipi anaweza zitumia ili apunguze kulala kwa muda mrefu ambapo kwa siku huenda ni zaidi hata ya masaa 8 ya kawaida.

  1. Habari,kuwa na usingizi wa muda mrefu na mzito sio Mara zote huwa ni tatizo. Na usingizi hutegemea na umri,kazi ama shughuli za mtu na hali ya afya ya mtu pia. Kuna sababu kadhaa husababisha hali hiyo kama endapo mtu ametumia kilevi kabla ya kulala na pia kuna baadhi ya dawa zinasababisha,hali ya kuwa na msongo wa mawazo.
   Pia hali hii imekuwa ikihusishwa na magonjwa kama ya kisukari,magonjwa ya moyo, kuumwa mgongo na kichwa . Hizi ni baadhi ya sababu kwa watu wengi.
   Ili kupata usingizi mzuri unaweza ukajijengea tabia ya kuwa muda maalum wa kulala na kuamka,usitumie vilevi au kahawa kabla ya muda wa kulala na pia hakikisha mazingira mazuri ya kulala chumba chenye huwa nzuri na malazi mazuri.

 6. je, MTU alieambukizwa gono inaweza kuchukua muda gani ili na yy aweze kuambukiza,,, au Mara tu baada ya kupata anaweza kuambukiza muda huo huo kama akikutana na MTU mwingine? au itachukua cku kadhaa ili na ww uweze kuambukiza

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show