Huduma ya kwanza kwa anaetokwa na damu puani

Kutokwa damu au kuvuja damu puani ni kati ya tatizo linalotokea kwa watu wengi katika maisha ya kila siku na hutokana na kupasuka kwa mirija midogo ya damu iliyoko puani.
Mara nyingi kuvuja damu huku sio hatarishi kwa maisha ila wakati mwingine huhitaji huduma ya haraka na pia kumuona daktari kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya visababishi:
Ajali au kupigwa ngumi puani ambapo huambatana na kuvunjika pua

Kuwa na mafua ya mara kwa mara

Kukwama kwa vitu puani kama karanga, harage au kutumia kidole wakati wa kujisafisha.

Kuwa na msukumo wa damu au presha.

Matumizi ya dawa za kulevya kupitia puani

Huduma ya awali unayoweza kumpa au kumuelekeza mtu anayetokwa na damu puani

-kugandamiza pua katika sehemu ya mbele kwa muda wa dakika kumi hadi kumi na tano


-kukaa au kumkalisha wima na kuinamia au kumuinamisha mbele ili kuepuka kumeza damu na kuzuia kuziba kwa pua pamoja na kuzuia kichefuchefu

-kutokuinamia mbele kwa muda mrefu baada ya damu kuacha kutoka, inabidi akae au ukae wima.

-Kama damu itaendelea kuvuja kwa zaidi ya dakika 30 baada ya kugandamiza pua ni vyema ukafika kituo cha Afya ili kumuona daktari kwa matibabu zaidi

-Kama damu itavuja tena kwa mara nyingine zaidi ya mara moja ni vyema ukawahi hospitali au kituo cha afya ili kupata matibabu zaidi

-Kama damu kuvuja puani kumetokana na ajali puani au kichwani muone au muwahishe mgonjwa katika kituo cha afya haraka

-Kama unajisikia au anajisikia kizunguzungu baada ya damu kutoka puani muwahishe au wahi katika kituo cha afya kwa matibabu zaidi.

Privacy Preference Center