Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka

Nyoka ni wanyama ambao ni hatari hasa pale wanapomg’ata mtu, lakini kuna uwezekano nyoka akawa mwenye sumu au asiwe mwenye sumu. Endapo nyoka aliyehusika akawa mwenye sumu basi chukua tahadhari, kwani huweza kusababisha kifo papo hapo au baada ya mda. Mtu aliyeng’atwa na nyoka anahitaji kuwahishwa kwenye kituo cha afya au hospitali haraka!

Ila wakati utaratibu wa kumpeleka hospitali ukifanyika ni muhimu sana kumpa huduma ya kwanza kama ifuatavyo:

  • Kwanza kabisa jitahidi utambue muonekano wa nyoka huyo kama ameonekana ili uweze kuelezea kwa wataalamu wa afya.
  • Kisha mtulize mwathirika asihangaike wala kutembea tembea, mlaze chali na hakikisha asiinue sehemu alipong’atwa juu zaidi ya usawa wa moyo. Hii itasaidia kupunguza sumu kusambaa mwilini.
  • Pia muondole wasiwasi ili kupunguza msukumo wa damu unaoweza kupelekea usambazwaji wa sumu husika mwilini kwa kiwango kikubwa.
  • Ondoa vitu vinavyobana kama pete au nguo za kubana kwenye sehemu iliyong’atwa kwani sehemu hiyo inaweza kuvimba.
  • Usifunge sehemu ya juu au chini ya alipong’atwa kwa nguo, kamba au kitu chochote kile kingine.
  • Usikate au kupasua sehemu iliyong’atwa kwa kisu au kiwembeย  na pia usijaribu kunyonya sumu kutoka kwenye sehemu iliyong’atwa kwa mdomo.
  • Usimpe kitu chochote cha kula wala usiweke barafu kwenye sehemu iliyong’atwa.
  • Pia angalia hali ya mgonjwa: mapigo ya moyo, upumuaji na joto la mwili. Kama anakuwa wa baridi mfunike ili aweze kupata joto.
  • Muwahishe kituo cha afya au hospitali iliyo karibu na wewe kwa ajili ya matibabu. Kamaย  nyoka aliyemng’ata yupo aliuliwa au kukamatwa, nenda naye katika kituo cha afya au hospitali pia.

Privacy Preference Center