Kutoboka kwa meno na sababu zake.

”Miongoni mwa matatizo ya kinywa yanayowasumbua watu wengi  ni hali ya jino kutengeneza tundu ambalo tundu hili lisipozibwa mapema huenda likasababisha maumivu makali na hatimaye jino kung’olewa”.

                     Nini basi inasababisha jino kutoboka????

Pale ambapo mtu anapokula chakula au kunywa kitu chenye sukari kwa wingi(aina ya sucrose) bacteria walioko mdomoni wanatumia sukari hii na kutengeneza tindikali(lactic acid) ambayo ndiyo inayosababisha meno kuoza au kutoboka.Ikumbukwe kuwa siyo vyakula vyenye sukari tu ndo husababisha meno kutoboka bali  hata vyakula vya wanga pia kwasababu navyo vinaposagwa hutengeneza sukari ambayo huchangia kuozesha meno.Mashambulizi haya huweza kuchukua hata lisaa limoja baada ya kuwa umekula vyakula hivi kabla ya madini ya chumvi yaliyoko kwenye mate kupambana na hali hii.

Kutoboka kwa jino sio kitu cha siku au mwezi bali ni kitu endelevu kinachochukua mpaka  miezi 18 na zaidi kwa tobo kutokea.Pia ni muhimu kufahamu kuwa sio ule wingi wa chakula chenye sukari ndio inayosababisha meno kutoboka kwa haraka bali ni mara ngapi kwa siku unatumia vyakula hivi.

  • Zipo dalili za maradhi haya ambayo ni jino husika kuwa na alama nyeupe kama ya chaki kwenye eneo linalotaka kutoboka.Alama hii  mara nyingi huonwa na daktari wa meno anapofanya uchunguzi wa  kinywa lakini weupe huu hauna tatizo kwa mhusika mpaka pale tundu litakapotokea na wengine hadi anaposkia maumivu ndio anagundua tundu hili.
  • Maumivu yanapoaanza inamaanisha kuwa tundu hilo limefika kwenye kiini cha jino(pulp) na maumivu haya huwepo mara nyingi mtu anapokula kitu cha baridi au moto au chenye sukari.Tiba inahitajika mapema pale tu mtu anapoanza kusikia maumivu ya jino ili kuepusha kung’olewa kwa jino pale ambapo madhara yamekua makubwa.

Wengi wetu tunasubiri hadi maumivu ya jino yakiwa makali ndo tukamuone daktari wa meno.HII SIO SAHIHI.Unapoona jino lako limetoboka hata kama halina maumivu ni vyema kumuona daktari mapema ili tundu hilo lizibwe na kuepusha madhara mengine

Ili kupunguza tatizo hili ni vyema kuepuka kula vitu vya sukari kwa wingi na hata pale utakapotumia vyakula hivi ni vyema kusukutua kwa maji masafi au kupiga mswaki kabisa kwa kutumia dawa ya meno yenye madini ya floridi.

Ni vyema kumuona daktari wa meno mara kwa mara ili matatizo haya yagundulike mapema na kutibiwa.

Meno yetu ni fahari yetu tuyatunze”.

 

 

 

10 thoughts on “Kutoboka kwa meno na sababu zake.

      1. Material yapo yaaina nyingi pamanent mfano GIC, COMPOSITE, na temporary ZINC EUGENAL NA IRM haya nimifano but yapo mengi sanaa

  1. Ushauri watu wawe natabia yakufanya oral medical check up Kwa kila six months ili kubaini hayo matatizo nakupewa Ushauri nini kifanyike Kwa wakati hip. Watanzania waliowengi wanaenda hospital akati anamaumivu makali yajino nakupelekea kulitoa. Wahi hospital ukapate Ushauri wa wataalamu maana si kila jino lakung’oa wajamenii.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show