Fahamu mazoezi muhimu kwa wazee( miaka 60 na zaidi)

Watu wazima/wazee wanaweza kufanya mazoezi ambayo yanasaidia kuimarisha afya zao pasipo kuleta madhara kwenye viungo vya mwili.
Haya ni baadhi ya mazoezi ya msingi:
1. Kutembea
2. Kukimbia polepole( jogging)
3. Mazoezi mepesi ya viungo
4. Kuogelea
5. Kuendesha baiskeli
Kumbuka bima namba moja ya afya ya mzee ni mazoezi.
Ni vyema kufanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kwa siku. Tenga siku 3 ndani ya wiki ambazo unaweza kufanya mazoezi.
Si vyema kwa wazee kufanya mazoezi magumu kama vile kubeba vyuma vizito. Hii inaweza kuleta athari mbalimbali kwenye viungo vya miili yao.

Privacy Preference Center