Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume au kike.

Kupata mtoto wa jinsia unayotaka ni moja ya changamoto na fumbo ambalo wengi huwasumbua.Kwa kutumia sayansi na mfumo wa binadamu inaweza kukusaidia kutatua fumbo hili,karibu tujifunze!!

Jinsia ya Mtoto

Mtoto hutengenezwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la kike. Mbegu za kiume hubeba vinasaba vya X na Y, wakati yai la mwanamke likiwa na vinasaba vya X peke. Ikikutana mbegu ya kiume yenye kinasaba cha X na yai la kike (yenyewe yana vinasaba vya X peke yake) mtoto wa kike hutungwa. Mbegu ya kiume yenye kinasaba cha Y Ikikutana na yai la kike, mtoto wa kiume hutungwa.

 • Mbegu ya kiume Y + Yai la kike X = Mtoto wa Kiume
 • Mbegu ya kiume X + Yai la kike X = Mtoto wa Kike

Njia za Kupata Mtoto Wa Jinsia Uipendayo

Mtoto wa kiume

Mbegu za kiume zenye vinasaba vya Y huwa ni nyepesi, husafiri kwa haraka katika via vya uzazi vya mwanamke na huishi kwa muda mfupi ukilinganisha na mbegu zenye vinasaba X. Zenye vinasaba X huwa nzito zaidi, huenda polepole na huishi kwa muda mrefu zaidi.

Hivyo, kinadharia ili kupata mtoto wa kiume unaweza ukakutana na mwenza wako siku ambayo yai la uzazi linatoka (ovulation), kwani mbegu Y zitasafiri haraka na kukutana na yai ili kulirutubisha kuwa mtoto wa kiume.Ila kwasababu ni ngumu kutambua ni lini yai linatoka hivyo unashauriwa kukutana mwenzi wako kilasiku katika zile siku za hatari.

Mtoto wa kike

Mtoto wa kike, kutana na mwenzi wako siku 2 au 3 kabla ya yai kutoka. Kwa sababu mbegu Y huishi kwa muda mfupi, nyingi zitakufa wakati zinasubiri yai huku mbegu X zikiwa kwa wingi mpaka siku yai linatoka. Yai likitoka mbegu X zitakuwa kwa wingi kuungana na yai kutunga mtoto wa kike.Ili kupata mtoto wa kike inabidi kukutana na mwenzi wako siku chache kabla ya yai kutoka na sio kilasiku.

11 thoughts on “Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume au kike.

 1. Shukrani kwa maelezo yako…

  Mie nina maswali mawili.

  1. Umesema kwa upande wa kiume kwakuwa mtu hana uhakika wa siku ya ovulation basi mtu ashiriki mapenzi siku zote. Sasa kwa mtoto wa kike umeshauri siku 2 au 3 kabla ya ovulation, sasa kwa kuzingatia ile dhana hapo juu ya mtu kutokuwa na uhakika huoni kwamba mtu anaweza akashiriki tendo kumbe ikawa sio siku 2 nyuma akaishi kupata mtoto wa kiume?

  1. Asante kwa kuchukua mda wako kujifunza nasi,
   kwanza kabisa ili uweze kufanikisha hili mwanamke inabidi achukue mda ili kujua ana mzunguko wa siku ngapi kwa kawaida ni 21-35 na pia mzunguko wako inabidi uwe ambao haubadiliki (regular) .Hivyo basi ukifanikisha hilo inakuwa rahisi kujua siku zako za hatari na siku ambayo utatarajia yai litoke,hivyo ili kupata mtoto wa kike utakutana na mwenzi wako siku ambazo zipo mbali na siku ambayo yai litatoka (ovulation)kama siku 3 kabla au mbili kabla na sio siku moja kabla au siku yenyewe.

 2. Swali langu la pili.

  Kuna dhana ya mababu zetu kuwa ukitaka mtoto wa kiume ule vyakula kama nyama na jamii hiyo na kwa mtoto wa kike ule samaki (hii ni kwa mwanamke)… Je dhana hiyo ina uhalisia ktk utaalam wenu wa kisasa?

  Kama ina uhalisia je naweza kupata maelezo ni kwanini imeshauriwa vyakula hivyo na uhusiano wake na kupata watoto wa jinsi husika?

  1. Asante kwa swali zuri,kwanza kabisa sijawahi kusikia kuhusu hizi imani ndio umenijuza nashukuru kwa hilo, ila sidhani kama zina uhalisia wowote katika hili swala kwasababu kwanza zote ni protini pili hamna uhusiano wowote katika utungaji wa jinsia ya mtoto na hivi vyakula.

 3. bhana bhana napenda kusema ahsante tu maana wengine wake zetu watarajiwa wanaeza kuwa madaktari wangeweza kutufanyia hila kila siku tiish wa kike..nashkuru kwa kusema tena ahsante..

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show