Kuelekea kufikia malengo yangu ya mazoezi(part 1)

 

Mazoezi ni muhimu kwa afya pale yanapofanywa mara kwa mara na kwa usahihi. Mazoezi yatakufanya mwenye nguvu Zaidi na kurefusha maisha. Ikiwa unafanyia mazoezi yako nyumbani, mahali pa nje ama gym, kuna vitu muhimu vya kufanya ili mazoezi yawe yenye matokeo yanayotarajiwa.

Vitu hivi huanzia kwenye maandalizi kabla ya kuanza mazoezini mpaka mazoezi yenyewe. Kwenye Makala hii nitaelezea sehemu ya mwanzo yaani maandalizi kati ya zile nyingi na muendelezo utakuwa katika Makala zitakazo fuatia.

Vifuatavyo ni vitu muhimu katika sehemu ya maandalizi. Kama ifahamikavyo kuwa katika hali nyingine  mwanzo  huwa ni mgumu ila unapofanikiwa mazoezi huwa yenye furaha;

  1. Vaa nguo sahihi za mazoezi ,zisizobana hasa katika maeneo ya jointi wala zile zinazothibiti kujitanua kwa mwili vya kutosha.
  2. Vaa raba sahihi, zinavokutosha vizuri, nyepesi na inashauriwa zenye soli pana
  3. raba zenye soli pana na nguo zenye nafasi
  4. Kunywa maji ya kutosha kabla ya kufanya mazoezi ,maji yatakusaidia katika kutanuka kwa misuli kipindi cha mazoezi na pia kuondoa harufu mbaya ya jasho.
  5. Usijinyooshe(stretching) kabla ya kuanza mazoezi hii ni kinyume na wengi waaminivyo .ila kujinyoosha kunaweza kuchosha misuli yako hata kabla ya mazoezi.
  6. Fanya mazoezi ya kupasha ,haya ni sawa kabisa na mazoezi unayoapanga kufanya ila unayafanya kwa nguvu ndogo Zaidi. Kwa mfano ;ukipanga kukimbia utaanza kwa kukimbia kwa spidi ndogo (jogging) halafu ndipo utaongeza mwendo.
  7. Uwe na malengo ya aidha kila wiki au kila mwezi ya matokeo yatokanayo na mazoezi unayofanya.
  8. Fanya mazoezi yanayokupa furaha na motisha Zaidi.
  9. Fanya mazoezi yatakayokuwa yanachangamsha sehemu nyingi za mwili wako.
  10. Onana na daktari kama una matatizo ya kiafya kama magonjwa ya pumu, mapafu, figo ,moyo na kadhakika, hii itakusaidia kupata ushauri sahihi wa aina ya mazoezi yanayoweza kufaa kulingana na hali yako. Vivyohivyo kama unapata shida wakati wa mazoezi kama kuishiwa pumzi ama kuchoka sana ,kuonana na daktari itakusaidia kujua hali yako ya afya na kuepusha magonjwa.

Iwapo ukiweza kufanya maandalizi mazuri, mazoezi yako yataenda vyema na hata kupata matokeo mazuri bila ya kuchoka wala kujiumiza. Tukutane wiki ijayo tukizungumza aina tofauti za mazoezi na faida zake mwilini.

 

Privacy Preference Center