Kuelekea kufikia malengo yangu ya mazoezi(part II)

 

Baada ya sehemu ya kwanza ya maandilizi ya mazoezi ,sehemu hii tunaona mazoezi yanayosaidia msukumo wa damu, na hivyo kuyafanya yawe bora sana hata kwa watu wenye matatizo ya moyo na kisukari na hata kusaidia kuepusha magonjwa haya kwa watu ambao wanaweza kuyapata mfano watu wenye uzito mkubwa.

Mazoezi haya huitwa Aerobics/Cardio, haya huongeza kasi ya mapigo ya moyo na kupumua ili kuongeza oksijeni kwenye misuli ya mwili. Mara nyingi hayatumii nguvu kubwa ila ni mazoezi yanayochukua muda mwingi. Kama jina lake “Aerobics” ni neno linalomaanisha enye oksijeni na hivyo husaidia usambazaji mzuri wa oksejeni mwilini na neno “Cardio” likimaanisha moyo kuwa mazoezi haya husaidia moyo kusukuma damu vizuri.

Ni rahisi kuona mabadiliko ufanyapo mazoezi haya na hutumia nguvu ndogo mpaka wastani . mazoezi haya ni kama yafuatayo;

-kutembea kwa mwendo wa wastani

-kukimbia kwa mwendo mdogo hii huwa tunaita jogging

-kupanda ngazi hii husaidia misuli yako ya miguu na huhitaji uangalifu kuepusha ajali

 

                     Kucheza dansi

-kucheza dansi,kuogelea na kuruka kamba,hii sio ya kujifurahisha tu husaidia misuli ya miguu na mikono.

Aerobics/Cardio ni mazoezi yanayokufanya utambue kabisa utumikaji wa oksijeni kwenye misuli kwa kuongeza kasi ya upumuaji na mapigo ya moyo. Ifahamike kuwa mazoezi haya hutumia nguvu ndogo na kufanywa kwa muda mrefu tofauti na kunyanyua vyuma ,kukimbia kwa kasi au kuvuta kamba haya hutumia nguvu kubwa na muda mfupi na huitwa “Anaerobic” haya tutazungumza kwenye Makala ijayo.

Mazoezi ya Aerobics hutujengea uwezo wa kuweza kufanya kitu kwa nguvu ndogo na kwa muda mrefu.

FAIDA ZA MAZOEZI YA AEROBICS

1.husaidia kupunguza uzito kwa kukata mafuta yanayozidi mwilini.

2.husaidia kupunguza msukumo  mkubwa wa damu

3.kuepusha hatari ya kupata magonjwa kama kisukari na presha ya juu

4.huepusha hatari ya saratani kama  saratani ya titi na utumbo mkubwa.

5.hupunguza msongo wa mawazo

6.humpa mtu muonekano mzuri kama mjengo mzuri wa misuli ya mwili.

”USICHOKE KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU KWA AFYA YAKO ”

2 thoughts on “Kuelekea kufikia malengo yangu ya mazoezi(part II)

  1. Asante kwa taarifa hii ila ningependa kujua utofauti wa kutembea kwa mwendo wa pole pole na mwendo wa kasi utofauti wake kwenye izo cardio

    1. Asante sana,mara zote kutembea ni zoezi la cardio yaaani aerobic. Kutembea kwa muda mrefu na spidi ya wastani (brisking)
      Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show