lini ulibadilisha mswaki?

 

Mswaki ย ni moja kati ya vitu vinavyoongoza kwa kusahaulika na watu wengi.Inasikitisha kuwa wengi wala hawajali kama mswaki alionao unafaa au hapana maana kwao ni โ€˜โ€™mswaki tu kwani nini?,lakini kwangu mimi mswaki ni moja kati ya vitu muhimu ambavyo niย  lazima nihakikishe ninao tena unaofaa.Watu wakisafiri wanasahau kubeba mswaki,Wakienda kununua mahitaji muhimu(shopping) wanasahau mswaki kwanza wala haupo kwenye hesabu,Hata akienda kulala kwa rafiki yake anasahau mswaki.Wengine wanatumia mswaki ambao umeshaharibika sana na hivo hauwezi kufikia lengo la kusafisha kinywa kwa usadifu.

Zifuatazo ni sifa za mswaki mzuri na unaofaa kwa matumizi ya kila siku ili kusafisha kinywa vizuri.

  • Inashauriwa kutumia mswaki laini siyo mgumu sana
  • Ni lazima uwe na brashi iliyosimama wima ili kuweza kufika maeneo yote ya kinywani
  • Uwe wa ukubwa unaolingana na kinywa cha mtumiaji mfano;mswaki mdogo kwa ajili ya watoto na usimlazimishe mtoto kutumia mswaki mkubwa utamletea karaha na kumuumiza wakati mwingine.
  • Ncha ya mwisho ya mswaki inaishauriwa kuwa na umbo la pembe tatu yenye uduara.Hii husaidia kufika maeneo ya nyuma kabisa ya meno ya mwisho na kuzuia kujigonga na kuumia kwenye nyama za ndani ya mdomo wakati wa kupiga mswaki.
  • Inashauriwa kubadilisha mswaki wako kila inapobidi usisubiri miezi mitatu ifike ukiona umeanza kupinda tu na brashi zimeanza kujipinda basi nunua mwingine.
brashi zilizosimama na laini
ncha ya mwisho ya pembetatu duara

 

Hebu fikiria kinywa chako ndio mlango mkuu wa kuingia mwilini mwako kwanini kiwe kichafu? Kwani mswaki una gharama kubwa kiasi gani mpka ushindwe kununua na kusubiri mpaka dawa iishe ndipo upate mwingine wa promosheni?Unaonaje tukianza leo kampeni ya kununua miswaki mipya,hebu mkumbushe rafiki yako na uwapendao kununa miswaki,unaweza hata kuwapatia mswaki kama zawadi.ANZA SASA KUNUNUA MSWAKI MPYA.


Flaviana Nyatu DDS 5 ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

A happy and passionate dental surgeon.

All author posts

Privacy Preference Center