Mambo gani ni muhimu kuzingatia kabla ya kuanza kufanya mazoezi?

Mazoezi ya viungo ni moja kati ya mihimili muhimu sana kwa ajili ya kujenga afya. Kufanya mazoezi bila kujua kanuni mbalimbali kunaweza kuleta madhara mbalimbali ya afya. Zifuatazo ni baadhi ya kanuni za kuboresha ufanyaji wa mazoezi

1: Anza kwa kupasha misuli na kujipooza kidogo kama mazoezi unayopanga kufanya ni ya muda mrefu
2: Jipange kuanza taratibu na ongeza uzito wa mazoezi kwa hatua kama ni mara yako ya kwanza
3: Kumbuka kwamba mazoezi mazito sana au mara nyingi sana husababisha madhara kama vile kuvimba kwa ukano, maumivu ya misuli na joint na hata kuvunjika mifupa hasa ile midogo midogo. Pia mazoezi ya aina moja kwenye baadhi ya viungo vya mwili pekee huweza kuleta madhara haya pia. Hivyo ni vema kuchanganya aina za mazoezi na kupumzika.
4: Usikilize mwili wako. Punguza au Acha mazoezi kwa muda kama ni mgonjwa ama unapata maumivu makali sana wakati au baada ya mazoezi.
5: Endapo utaacha mazoezi kwa muda, rejea kwa kuanza mazoezi rahisi mwanzoni kabla ya kurudia mazoezi yako ya kawaida
6: Kunywa maji mengi hutosheleza kurudisha mwili katika uwiano mzuri wa vimiminika, ingawa watu wengine huweza kuhitaji madini kadhaa katika maji (electrolytes)
7: Chagua mavazi yanayoendana na aina ya mazoezi unayofanya ili uwe huru.
8.Kwa mazoezi yanayohitaji nguvu nyingi,hali ya mwili kuwa vizuri ni jambo la muhimu, kwa mara ya kwanza ya mazoezi usitumie vifaa vizito kwanza endapo bado unajifunza namna ya kuyafanya mazoezi haya. Endelea na uzito mwepesi kadri siku zinavyoendelea utaongeza kadri ya hali yako. Usiikimbilie kufanya mazoezi ya kifua au misuli ya mikono na miguu haraka haraka hata kama mwili wako upo katika hali nzuri kimazoezi.
9:Kufanya mazoezi mazito sana wakati wa joto husababisha madhara kama mwili kupata joto sana na kukaukiwa maji hivyo ni vema kufanya mazoezi kulingana na hali ya hewa husika
Madhara haya huambatana na dalili kama vile :
Maumivu ya kichwa, kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio, kichefuchefu hata kuzimia.

10: Vaa mavazi sahihi kulingana na hali ya hewa kuepuka adhari za mwili zitokanazo na kutokuvaa mavazi sahihi katika hali za hewa mbalimbali

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center