Mazoezi ni dawa

Tumeona jinsi ambavyo mazoezi husaidia mifumo mbali mbali ya mwili kufanya kazi vizuri pia katika kusaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama:
1. Kisukari
2. Magonjwa ya moyo
3. Shinikizo la damu
4. Kuongeza kinga za mwili n.k
Kwa kuwa mazoezi ni dawa ni muhimu kuyatumia kwa kufuata dozi kama dawa tulizozizoea.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia ukiwa mwana mazoezi;
1. Kwa ujumla mtu anapaswa kufanya mazoezi walau siku tatu mpaka nne kwa wiki kwa dakika 20 hadi 30 kwa siku.
2. Mazoezi hayo yawe mchanganyiko wa mazoezi ya misuli na ya kuongeza pumzi (cardio).
3. Ni muhimu kuwa na mfumo wa mazoezi ambao kuna siku za kupumzika ili kuipa misuli ya mwili muda wa kurudi katika hali imara zaidi.
4. Ni muhimu kupata kitu cha sukari kama ndizi nusu saa kabla ya mazoezi ili kuepuka kuishiwa nguvu wakati wa mazoezi.
5. Ni muhimu kunywa maji ya kutosha ukiwa mtu wa mazoezi maana unapoteza maji sana wakati wa mazoezi kama jasho.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center