Ni sahihi kwa mgonjwa wa figo kufanya mazoezi?

Mazoezi kimwili ni muhimu sana katika dunia ya leo. Kila mtu anafurahia faida za mazoezi. Mazoezi hufanya mwili wako uwe na nguvu na wenye afya.

Naweza kushiriki katika mazoezi nikiwa na ugonjwa wa figo?
Ndiyo. Watu ambao wanaamua kufuata mpango wa mazoezi huwa na afya bora zaidi.

Mazoezi haya yatanipa faidia gani kama mgonjwa wa figo?

  • Udhibiti bora wa shinikizo la damu
  • Kupunguza kiwango cha mafuta katika damu (cholesterol na triglycerides)
  • Kuboresha na kuimarisha misuli ya mwili
  • Usingizi bora
  • Udhibiti bora wa uzito wa mwili

Je, ninahitaji kumuona daktari wangu kabla ya kuanza mazoezi?
Ndiyo. Kabla ya kuanza mpango wowote wa zoezi, hakikisha uonane na daktari wako.
Wakati wa kufanya mipango ya mazoezi, mtazingatia pia:

  • Aina ya zoezi
  • Muda utakaotumia kufanya mazoezi
  • Ni mara ngapi utayafanya

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center