HOMA YA INI.

Homa ya ini B ni yabisi kavu ya ini (kuvimba kwa ini) kunakosababishwa na kirusi cha aina ya B (hepatitis B virus) . Homa ya ini ina dalili ya maumivu makali ya tumbo la juu upande wa kulia, kukosa hamu ya kula, homa za mara kwa mara, macho kuwa ya njano, mkojo kuwa mweusi, kupungua uzito kwa ghafla.
Kirusi hiki husambazwa kwa njia tofauti hasa hasa kwa njia za majimaji ya mwili kama inavoelezewa hapa chini
1: Kupitia mate, Mate ya mtu mwenye homa ya ini hubeba virusi hivi vya aina B. Hivyo inapotokea mtu mwingine akayagusa kwa njia yoyote anaweza akaambukizwa. Kama kuchangia kijiko ambacho hakijaoshwa vizuri.
2: kupitia majimaji ya sehemu za siri. Watu wanapojamiiana bila kinga inaweza kusambaza ugonjwa huu kwa sababu virusi hukaa kwenye maji maji haya. Hivyo hatakuwa na wapenzi wengi kunamuweka mtu kwenye hatari ya kutata ugonjwa huu.
3:Damu ambayo inavirusi hivi husambaza homa ya ini kwa haraka zaidi. Hivyo ni sahihi zaidi kujiepusha kugusa damu ya mtu mwingine.
Kuna chanjo ya homa ya ini, ingawaje inapatikana sehemu chache sana, unaposikia kuna hii chanjo jitokeze kwa haraka.

1 thought on “HOMA YA INI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.