Je, unasumbuliwa na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi?

Moja kati ya matatizo mengi ambayo huwakumba wanawake na wasichana wengi siku hizi ni kupata maumivu ya tumbo wakati wa hedhi. Hii hujulikana kama tumbo la hedhi na kitaalamu huitwa Dysmenorrhea. Maumivu haya hutokea pale misuli ya kuta za kizazi inapotanuka na kubana mishipa ya damu hivyo kuzuia usambaaji wa damu kwenye misuli hiyo.

Haya ni maumivu yanayotokea hasa chini ya tumbo au kiunoni pale mwanamke anapokuwa katika siku zake ,aidha anapoanza kupata siku au siku chache kabla ya kupata siku zake. Mara nyingi huwa ni masaa 48-72 kabla au baada ya kupata hedhi.

Maumivu haya hutofautiana kwa wanawake wengi  kuanzia kutokuwa makali sana mpaka kuwa makali yasiyovumilika. Na pia huambata na kichefuchefu, kujisikia kutapika, kuharisha, maumivu sehemu za chini ya mgongo na hadi mapajani, kupata maumivu ya kichwa na kuchoka sana.

Kuna aina mbili za maumivu haya ya hedhi ,kama ifuatavyo

  1. Aina ya kwanza(Primary dsymenorrhea) ;haya ni maumivu yasiyohusishwa na magonjwa yoyote wala sababu za kitiba . mara nyingi maumivu haya hutokea miaka michache baada ya kuanza kupata hedhi na huwapata mpaka 50% ya wanawake waliokwisha pevuka. Hapa wanawake wengi huhisi maumivu chini ya tumbo na kiunoni na maumivu haya huanza siku 1-2 kabla ya hedhi na huweza kwenda mpaka 2-4 baada ya kuanza hedhi.
  2. Aina ya pili(Secondary dysmenorrhea) ;haya ni maumivu yanayojumuisha uwepo wa magonjwa kama magonjwa ya nyonga, matatizo katika kizazi au matatizo katika mirija ya mayai.

 

Sababu zinazoongeza hatari ya uwezekano wa maumivu haya ni kama ifuatavyo kwa aina ya kwanza,

1.Kuvunja ungo katika umri chini ya miaka 12

2.Kupata damu nyingi kuliko kawaida au kupata hedhi kwa muda mrefu.

3.Wanawake ambao hawajazaa

4.Kuwa na uzito mkubwa kuliko kawaida

5.Uwepo wa historia ya kupata maumivu ya hedhi katika familia

6.Uvutaji wa sigara

       Kwa aina ya pili;

1.Ugonjwa wa endometriosis ,pale ambapo seli za ukuta wa kizazi kukua katika sehemu zingine kama kwenye mfuko wa mayai au mirija ya mayai.

2.Magonjwa  ya nyonga au uwepo wa uvimbe.

3.Magonjwa ya zinaa yatokanayo na bacteria.

UFANYE NINI UKIPATA MAUMIVU HAYA

-Unaweza kuweka kitambaa chenye maji ya uvuguvugu au kujikanda na chupa ya plastiki yenye maji ya uvuguvugu chini ya tumbo au unaweza kuoga maji  ya uvuguvugu.

-usitumie vitu vyenye chumvi nyingi,sukari nyingi au kahawa wakati wa hedhi.

-jikande taratibu  tumboni  na mgongo inaweza kukupunguzia maumivu.

-kutumia dawa za maumivu kama panadol na ibuprofen pale maumivu yanapozidi.

Tafiti zinaonyesha kuwa kwa wanawake wenye tabia ya kufanya mazoezi ya viungo ,asilimia kubwa huwa hawapati maumivu ya hedhi. Hivyo basi inashauriwa kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya viungo kama sehemu ya ratiba yako.

Ni wakati gani umuone daktari?

Pale unapofanya njia zote zilizotajwa  na bado maumivu yakawa yanaongezeka au dalili za kutapika sana na hata kupoteza fahamu.

 

4 thoughts on “Je, unasumbuliwa na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi?

    1. Haswaa,maumivu hao kwa wengine huhusisha kichwa kuuma kama nilivyotaja na dalili zinginezo kama uchovu na kuishiwa nguvu miguu kwa baadhi ya watu

    1. Kwa tafiti zilizofanyika maumivu hayo hupungua ama kuisha kabisa kwa asilimia kubwa ya wasichana/wanawake pale wanapozaa kwa sababu misuli inakuwa imetanuka kidogo na hivyo sio rahisi kugandamiza mishipa ya damu japokuwa bado kuna asilimia ya watu hupata

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show