UTOAJI WA MIMBA USIO SALAMA

UTOAJI MIMBA USIO SALAMA.

  • Tanzania ni kati ya nchi zenye uwiano wa juu wa vifo vya wajawazito duniani na utoaji mimba usio salama ni moja kati ya sababu zinazoongoza kwa takribani robo moja ya vifo ya uzazi.
  •  Sheria na sera ya utoaji mimba nchini Tanzania huidhinisha utoaji mimba Kwa dhumuni la kuokoa maisha ya mwanamke, tofauti na hapo utoaji mimba ni kosa la jinai. Kutokana na hofu hii ya kushtakiwa kumekuwa na ongezeko kubwa la utoaji mimba usio salama.

Utoaji mimba usio sahihi ni upi?

Utoaji mimba usio salama huusisha hatua zozote anazochukua mama mjamzito kusitisha ujauzito wake unaofanywa na mtu asiye na ujuzi sahihi au katika eneo lisilo na huduma sahihi za Afya au vyote viwili(WHO)(1)

Njia mbalimbali hutumika katika utoaji mimba usio salama zikiwemo matumizi ya mitishamba,sabuni na kemikali,vijiti na vitu vya ncha kali, majivu au matumizi ya vidonge kama misoprostol.

Madhara gani mtu hupata kwa kutoa mimba kusiko salama?

Madhara yatokanayo na utoaji mimba usio salama hutokana na sababu kadhaa zikiwemo;

• Kubaki kwa masalia ya mimba ndani ya mji wa uzazi.

• Mji wa uzazi kushindwa kukakamaa mara baada ya kutoa mimba hivyo kusababisha damu nyingi kutoka.

• Maambukizi yanayotokana na vijidudu mbalimbali vinavyoingia katika mji wa uzazi wakati wa kutoa mimba ambavyo huweza kusambaa mwili mzima kuleta maambukizi ya vijidudu hivyo kwenye damu

• Kuumia au kutoboka kwa viungo vya mwili Kama vile mji wa mimba, kibofu cha mkojo,utumbo,na hata figo kunakosababishwa na matumizi ya vitu venye ncha kali katika kutoa mimba Kama vile vijiti

Je nitazitambuaje dalili hatarishi za utoaji mimba usio salama?

Dalili hatarishi ambazo hutokea baada ya utoaji mimba usio salama huusisha dalili moja au zaidi kati ya zifuatazo;

• Maumivu makali chini ya kitovu

• Kutokwa damu nyingi katika uke

• Homa( joto mwilini)

• Damu kutoka katika njia ya haja kubwa au ndogo mtu anapojisaidia

• Kichefuchefu na kutapika

Nifanye nini nionapo dalili hizi?

Katika hospitali na vituo vya afya zipo huduma mbalimbali sahihi za kuweza kuokoa maisha ya binti au mwanamke aliyepata madhara ya utoaji mimba usio sahihi. Ni vyema hivyo kuwahi katika kituo cha afya kilocho karibu nawe.

Kutoa mimba kunaweza kuepukika endapo njia sahihi za uzazi wa mpango zitatumika ili kuepuka mimba zisizotarajiwa. Elimu sahihi ya afya ya uzazi kama vile mwanamke kuujua vizuri mzunguko wake wa hedhi kunaweza pia kusaidia kuepuka mimba zisizotarajiwa na hivyo utoaji mimba hatarishi.

Kwa wanawake wenye viashiria vya kutoa mimba kulinda afya ya mama; taarifa hizi hutolewa hospitali na wataalamu na hufanyika katika usimamizi wao kuepuka madhara yoyote yatokanayo na utoaji mimba. Viashiria vya kutoa mimba kulinda afya ya mama huusisha ;

• Kuwa na presha ya juu sana isoyowezekana kudhibitika wakati wa mimba ambayo huhatarisha maisha ya mama

• kifafa cha mimba kisichodhibitika hivyo kuhatarisha maisha ya mama

na mengineyo

 

References

1.Unsafe abortion – World Health Organization

www.who.int › reproductivehealth › topics

2.Utoaji Mimba na Huduma baada ya Kuharibika kwa Mimba Nchini Tanzania | Guttmacher Institute:https://www.guttmacher.org/fact-sheet/utoaji-mimba-na-huduma-baada-ya-kuharibika-kwa-mimba-nchini-tanzania

1 thought on “UTOAJI WA MIMBA USIO SALAMA

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center