Je mtu mwenye kisukari anaweza kupata magonjwa ya kinywa!?

Kisukari ni ugonjwa ambao una madhara kwenye kila sehemu ya mwili wa binadamu,makala hii itaeleza matatizo ya kinywa na meno wanayoweza kuyapata wagonjwa wa kisukari na namna gani wanaweza kujikinga nayo.

Wagonjwa wa kisukari wanakabiliwa na matatizo kama;

 • Magonjwa sugu ya fizi(periodontal diseases); wagonjwa wa kisukari wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya fizi hasa wale ambao hawazingatii tiba ya kisukari magonjwa haya yanaweza kuanzia kutoka damu kwenye fizi, kukusanyika ugaga kwenye meno, kutengeneza vifuko kati ya jino na fizi(periodontal pockets), kutunga usaha kwenye fizi(periodontal abcess), kulegea kwa meno hata kuanguka kwa meno.
 • Kukaukiwa na mate mdomoni(xerostomia); mgonjwa anaweza kuskia ukavu na kama anaungua mdomoni, wengi wanakaukiwa na mate hivo kufanya wawe na hatari kubwa ya kuoza meno/kutoboka meno na kufanya watake kunywa maji mara kwa mara.
 • Kuchelewa kupona kwa pengo kama watang’olewa jino; inashauriwa mgonjwa kumtaarifu daktari wa kinywa na apimwe kiwango sukari kabla ya kung’oa jino.
 • Fangasi za mara kwa mara mdomoni(oral candidiasis), vidonda vya kujirudia mdomoni(apthous ulcers), upatapo hali hii wasiliana na wataalamu kupata msaada.
 • Kutoboka kwa meno; wagonjwa wengi hutoboka meno maeneo ya maungio ya sehemu ya nje ya jino na sehemu inayofunika mzizi wa jino(cervical caries) ambayo huwa inaleta changamoto sana hata kwenye matibabu ya kuziba hivo inashauriwa mgonjwa kuzingatia sana asipate shida hii mara nyingi kuziba kunashindikana hivo jino hung’olewa.
 • Kupoteza uwezo wa kuhisi ladha ya chakula; hii inaweza kuchangiwa na kutokuwa na kiwango cha mate cha kutosha mdomoni.

Inashauriwa mgonjwa wa kisukari kuzingatia yafuatayo ili kujikinga na matatizo haya

 1. Zingatia kutumia dawa za kisukari kwa uhakika kama ulivyoshauriwa na madaktari
 2. Kama Unahitaji kutibiwa meno mtaarifu daktari wa meno mapema kabla ya matibabu kuwa una kisukari
 3. Hakikisha umekula vizuri na kutumia dawa zako kabla ya kwenda kutibiwa meno hii itakupunguzia hatari ya kushuka kwa sukari wakati wa matibabu.
 4. Ikiwezekana omba kupangiwa kutibiwa asubuhi na toa ushirikiano mzuri kwa daktari ili matibabu yasichukue muda mrefu sana.
 5. Jenga tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa kinywa na meno mara kwa mara ili kuwahi kutibu magonjwa haya mapema kabla hayajawa na madhara makubwa.

Zingatia afya yako, nenda kliniki na tumia dawa za kisukari kama ulivyoshauriwa ili kuepuka madhara ya kisukari.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center